Makumbusho ya Taifa la Tanzania inatarajia kuwa na programu maalum ya kimakumbusho yenye vionjo vya Kiswahili kama sehemu ya zao jipya la kivutio cha utalii wa utamaduni.

Akizungumzia Programu hiyo ya Kimakumbusho itakayofanyika Agosti 6,2022, Kijiji Cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga amesema jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuutangaza utalii nchini hususan kupitia Filamu ya The Royal Tour zinapaswa kuungwa mkono kwa kila namana hivyo wameamua kufanya hivyo kwa kuanzisha zao jipya la utalii ili kutoa fursa kwa watalii wa ndani na nje kufurahia utamaduni wa Kitanzania.

Dk.Lwoga ameongeza kuwa Tanzania ni tajiri wa urithi wa utamaduni ambao Taasisi anayoiongoza kupitia Kijiji cha Makumbusho inahusika katika kuhifadhi na kuipa jamii ya ndani na nje nafasi ya kufurahia uhifadhi ya Urithi huo wa asili hasa kwa kupitia program ya Kiutamaduni.

Aidha, Dk.Lwoga ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kwenye program hiyo itakayopambwa na ngoma ,muziki wenye maadhi ya Pwani, vyakula vya asili, masimulizi, Majigambo pamoja na Mavazi ya asili.

By Jamhuri