Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia,Dar es Salaam

Tanzania imepokea ugeni wa jopo la wataalamu likiwa limeambatana na wawekezaji na viongozi wa Serikali kutoka Jimbo la Changzhou Nchi China ambao wameonesha nia ya kuwekeza kwa kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo power tila,vifaa vya matrekta,vifaa tiba, bidhaa za umeme,water pump.

Akizungumza leo Machi 27, 2024 jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Sempeho Manongi amesema ugeni huo umekuja kutoka jimbo ambalo limeendelea sana kiviwanda na viwanda vyao vimetumia teknolojia ya hali ya juu hivyo utaalamu wao na uzoefu katika uendeshaji na uwekezaji ndiyo umesaidia kuelewa fursa zilizopo baina ya nchi hizi mbili.

“Siku ya leo tumefanya mazungumzo nao na katika mazungumzo kati yetu na wageni hawa na tumefahamu kuwa kuna maeneo yanashabinaa uwekezaji baina ya nchi hizi mbili hivyo sisi tumewaonyesha maeneo ya mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo,maeneo ya uzalishaji madini ya viwandani ambayo ni muhimu ” amesema Manongi

Sambamba na hayo kwa kuwa Shirika la Maendeleo (NDC) lina maeneo makubwa ya uwekezaji ikiwemo Kilimanjaro Machinine tools,Tange kule Tanga,Tamko Kibaha hivyo wapeoneshwa kuangalia fursa zilizopo .

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni iliyokuwa mwenyeji wa wawekezaji hao Anna Nyangasa kutoka Kampuni ya Canqus energy Solute (Amec Group) amesema wawekezaji wanakwenda kuwekeza mtaji wa kiasi tofauti tofauti katika kila eneo akitaja maeneo hayo Viwana vya kuzalisha mashine za kilimo wanawekeza Dola milion 24.5 za kitanzani ,Vifaa vya hospitali dola milion 6,vifa vya umeme dola milion 2,vifaa vya ujenzi dola milion 11.3 vifaa vya uchakataji mafuta dola milion 43.

Naye Mwakilishi wa wawekezaji hao kutoka nchini China Shein Dong ameshukuru kwa kupokelewa vizuri Tanzani na kutembezwa maeneo mbalimbali yenye fursa hivyo anaimani na nchi hii kwani wanahistoria ya miaka mingi iliyowekwa na viongozi waliopita hivho mashirikiano yataendelea siku hadi siku

Please follow and like us:
Pin Share