Charles Hilary (66), ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, amefariki dunia.
Hilary amefariki alfajiri ya leo na taarifa kutoka kwa watu wa karibu wamesema ameugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa Hospitali kwa matibabu.
Enzi za uhai wake, Charles Hilary aliwahi kuitumikia Redio Tanzania (1981 – 1994) na baadaye kujiunga na Radio One Stereo hadi mwaka 2003 alipoenda Ujerumani kujiunga na Radio Deusch Welle (DW).
Baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Idhaa ya Kiswahili na ilipofika mwaka 2015 alirejea nchini na kujiunga Azam Media ambako alifanya kazi hadi mwaka 2023 na baadaye aliuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Ikulu ya Zanzibar.
