Na Isri Mohamed

Beki wa kati wa Brazil, Thiago Emiliano Da Silva, ameagwa rasmi na klabu na wachezaji wenzake usiku wa kuamkia leo, mara baada ya mkataba wake kumalizika na kutoongeza kandarasi ya kusalia klabuni hapo.

Silva ambaye amedumu Chelsea kwa misimu minne mfululizo, katika hafla hiyo fupi ya kumuaga, yeye na familia yake walipata ‘Guard of Honor’ kama heshima kutoka kwa wachezaji wenzake.

Silva mwenye umri wa miaka 39, raia wa Brazil tayari ameshasaini mkataba na atajiunga na klabu ya Fluminense iliyopo nchini Brazil.

Silva ni miongoni mwa walinzi bora zaidi wa kizazi chake, anajulikana kwa uhodari wake wa ulinzi, nidhamu na uongozi.

Mafanikio makubwa aliyoyapata Da Silva akiwa Chelsea ni pamoja na kuchukua ubingwa wa Uefa Champions League na Uefa Super Cup (2021).

By Jamhuri