Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dodoma

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye mlengo wa hasa au chanya Kwa manufaa ya jamii

Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Rais wa Tanganyika Law Society ( TLS), Deus Nyabili alipokuwa akifungua mkutano wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu uhuru wa kujieleza ulioandaliwa na taasisi hiyo jijini Dodoma.

Nyabili amesema waandishi wa habari kama wataitumia vizuri Sheria ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ,yenye kuwataka kuwa huru kutangaza mambo mbalimbali ambayo yanafanyika kwenye jamii hata kama Iko kwenye mtazamo hasi itasadia kuleta mabadiliko.

“Mfano wa habari yenye kutoa uamuzi kutoka kwa viongozi na ukiangalia hauendani na uhuru wa habari wa wananchi kujieleza, bila kusita andika uhalisia kwamba hayo sio mawazo ya wananchi ”amesema.

Amesema lengo kuu la TLS ni kuwapa elimu
wanahabari na kubasilishana uzoefu, kutokana na yale ambayo tunayafahamu katika Katiba Ibara ya 18 inayosema kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zake mbele ya wengine na hilo ni jambo muhimu sana,

” Haki ya kujieleza sio tu ya kikatiba bali kila mtu anazaliwa nayo” haina mipaka kwa sababu lazima utumie hiyo haki kutoa maoni yako pale ambapo unaona inafaa” amesema.

Amesema wakati mwingine katika kutafuta ukweli kuna vikwazo mbalimbali, lakini ukiandika vizuri na kama ni ukweli utaona unawagusa watu furani hasa viongozi watawajibika tu kama ni wasikivu na wanataka mabadiliko.

Mwandishi wa habari mkongwe na mwezeshaji, Kajubi Mukajanga amewataka waandishi wa habari ,kusoma katiba na Sheria mbalimbali zinazowahusu ili wawe huru na kujiamini katika utendaji wa kazi zake za kila siku

Amesema waandishi lazima wajue haki ya uhuru wa kujieleza kuwa ni haki ya kila mtu na ina mruhusu kufanya mawasilisho bila ya kuingiliwa kwani ipo kwenye katiba na pia wanatakiwa kueneza elimu kuwa kila mtu anayo haki ya kupata taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu na shughuli za kijamii.

Selemani Pingoni ni Mkuu wa Idara ya Tathimini na Ufuatiliaji TLS, amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na makundi ya wanasheria na waandishi wa habari kuhusu haki ya kujieleza.

“Unajua miaka michache iliyopita nchi yetu ilipitia Sheria mbalimbali kuhusu vifungu vya Sheria, kulikuwa na malalamiko kutoka Kwa wadau mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Azaki wakieleza kutoridhishwa kwao na namna haki yao ya kutoa maoni kwa kiasi fulani ilikuwa unaminywa na Sheria”amesema .

“Sasa kuanzia hapo TLS ilikuwa na mpango wa kupitia sheria mbalimbali, ambazo zinaongoza masuala ya haki za kujieleza, tulizifanyia uchambuzi na kubaini mapungufu yake na kuanzisha mchakato ulio wahusisha wenye mamalka za juu ili kuona sheria hizi zinafanyiwa marekebisho.
xxxx