Mtakumbuka Mei 30,2024, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kushikiliwa Askari Polisi wanne (4) kwa ajili ya uchunguzi. Askari hao walikuwa wanafanya kazi kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Baada ya uchunguzi kukamilika ilibainika kuwa, askari hao walikuwa wamefuta picha kutoka kwenye camera za Jeshi la Polisi walizokuwa wanatumia kupima mwendokasi (speed rader) wa madereva waliokuwa  wamekiuka sheria za usalama barabarani kwa maslahi yao binafsi.

Walishtakiwa kijeshi na wakapaatikana na hatia na Julai 8,2024 walifukuzwa kazi na kufutwa Jeshini.

Imetolewa na:                                                              

David A. Misime – DCP

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi

Dodoma,Tanzania