*Alidaiwa kuchukuliwa nyumbani usiku bila ushahidi wa viongozi wa kijiji

*Polisi wakiri kufungua jalada la shambulio, uchunguzi waendelea

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Serengeti

Josephat Chagamba (28), mkazi wa Kitongoji cha Nyigoti, Serengeti mkoani Mara, amelala nyumbani akiwa katika hali mbaya baada ya kudaiwa kupigwa kufuatia tuhuma za wizi wa mbao.

Familia yake inasema kwa sasa kijana huyo, ambaye ni fundi mwashi, hawezi kukaa, kusimama, kutembea wala kuzungumza na analishwa kwa mrija.

Pia inadai anakojoa damu na ana majeraha sehemu mbalimbali za mwili, ikiwamo mgongoni na makalioni.

Tukio linadaiwa kuanzia saa 9 usiku wa Agosti 22, 2026, baada ya Mwinoki Machota, maarufu Mama Maria, kufika nyumbani kwa Chagamba na kugonga mlango.

Mama mzazi wa Chagamba, Mwajuma Ginawa, ameliambia JAMHURI kuwa mwanawe alipofungua mlango alikamatwa na mtu anayeitwa Barusi, anayefahamika katika eneo hilo kama mgambo.

“Barusi, Mama Maria na Elizabeth Joseph, maarufu Mama Baby, walimchukua mwanangu wakidai anatuhumiwa kuiba mbao za Mwinoki, yaani Mama Maria.

“Ilinipa shaka jinsi walivyokuja kumchukua usiku huo, hivyo tukaamua kufuatilia kujua wanampeleka wapi,” amesema Mwajuma.

Kipigo chadaiwa kuwa kikali

Mwajuma anadai mwanawe alipigwa katika maeneo mbalimbali ya mwili baada ya kuchukuliwa nyumbani, na tangu hapo afya yake imezorota.

KWA HABARI ZA KINA ZAIDI SOMA GAZETI LA JAMHURI LA SEPTEMBA 29 – HADI OKTOBA 5, 2026