Na Mussa Augustine, JamhuriMedia

Taasisi ya Hananja Compasion Foundation kwa Kushirikiana na Manispaa ya Ubungo inatarajia  Juni 24 Mwaka huu kwa ajili ya Kuhamasisha Wananchi kuchangia Damu kwa hiari huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Hashim Komba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Taasisi ya Hananja Compasion Foundation,  Richard Hananja amesema kwamba kongamano hil litafanyika katika centa ya Goba Manispaa ya Ubungo ambapo amewasihi wananchi kujitokeza Kwa wingi kuchangia damu kwa ni sadaka kwa wagonjwa waliopo hospitalini.

Hananja ambaye pia ni mchungaji mstaafu amesema kuwa wagonjwa waliopo hospitalini wanaohitaji damu ni wengi akitolea mfano wakina mama wajawazito wanaopoteza maisha wakati wa kujifungua pia madereva wanaopatwa na ajari hivyo ni jambo la kumpendeza Mungu kuchangia damu kuokoa masiha ya wengine.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wananchi wa Goba na maeneo mengine waje siku hiyo wachangie damu kwa hiari kwani ni sadaka, pia tunatoa elimu kwa Jamii kuondokana na imani potofu kuhusu uchangiaji wa Damu,ambapo Kongamano hili limebeba ujume wa “Changia Damu Salama ,Okoa Maisha ,Goba na damu salama”amesema Hananja.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani, makamu wake  Dkt.Philip Mpango pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa inatekeleza kaulimbiu yake ya Kazi iendeleee hivyo vifo vitokanavyo na upungufu wa damu vinasababisha kupoteza nguvu ya Taifa nakwamba jamii iwe na utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari ili kuwa na damu ya kutosha hospitalini.

Naye Mratibu wa Damu Salama Manispaa ya Ubungo Analimi Machalo amesema kwamba ongamano hilo nila mara ya kwanza kufanyika katika kata ya Goba lakini wanatarajia kukusanya Uniti 300 za Damu.

“Kumekuwa na uhitaji mkubwa wa damu hospitalini hivyo Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana nna wadau Mbalimbali tumekuwa tukihamasiha jamii kua na utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya ndugu zao, au watu wengine wenye uhitaji wa damu”amesema Machalo.

Pia Mratibu wa Mradi wa “Afya Yangu” kutoka shirika la Jhpiego USAID Joyce Francis Ishengoma amesema kwamba shirika hilo limekuwa likishirikiana na Wadau Wengine kama Taasisi ya Hananja Compasion Foundation kuhakikisha wanatoa huduma za afya zilizo bora kwa jamii.

“Wakina mama wajawazito wanapoteza Damu nyingi wakati wa kujifungua,wengine wanapata ajari na kutokwa damu nyingi hadi kupotezMaisha ,hivyo sisi kama Jhpiego USAID kupitia mradi wa Afya Yangu tunaotukeleza katika Kanda ya Dar es salaa,Tanga na Tabora tunashirikiana kuweka mazingira ya huduma bora za afya ili kuimarisha afya ya Mama na Mtoto” amesema Joyce.

Kikao hicho kilifanyika katika shule ya Sekondari Goba kawa ajili ya kuweka maandalizi ya kongamano hilo kimehudhuliwa na Viongozi wa Chama,Walimu pamoja na madereva wa bodaboda

By Jamhuri