Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa ambayo imesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, Serikali haijalala iko imara hivi karibuni itarekebishwa na kujengwa barabara kwa kiwango cha lami.

RC Chalamila amesema katika mkoa huo kila wilaya barabara zitajengwa ikiwemo Ilala Km 55.27, Ubungo Km 54.27, Kigamboni Km 42.11, Temeke Km 52.71, na Kinondoni Km 48.33 ambapo ametoa rai kwa wakandarasi wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi nzuri waombe kazi hiyo mara tu itakapo tangazwa.

Aidha RC Chalamila amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anadhamira ya dhati katika kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi katika nyanja anuai, hivyo amewaomba wananchi kuwa watulivu kutokana na kadhia wanayoipata ambayo imesababishwa na uhalibifu wa barabara katika maeneo yao kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha

By Jamhuri