Home Kitaifa Ummy Mwalimu Asifia Benk ya NMB Kwa Kutoa Elimu ya Fedha kwa Watoto, Wazazi na Vijana

Ummy Mwalimu Asifia Benk ya NMB Kwa Kutoa Elimu ya Fedha kwa Watoto, Wazazi na Vijana

by Jamhuri

Mkurugenzi Mtendaji Wa NMB Tanzania, Ineke Bussemaker(wa kwanza kulia) akizungumza katika hafla hiyo.

Waziri Wa afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto,Ummy mwalimu akizungumza katika uzinduzi huo.

Baadhi ya Wanafunzi wakiimba ngonjera mbele ya mgeni rasmi, waziri Ummy wakati wa hafla hiyo.

Mmoja wa wanafunzi walioshiriki uzinduzi huo akikabidhiwa daftari zilizotolewa na NMB katika hafla hiyo.

Baadhi ya Wanafunzi walioshiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.

 

Waziri Wa afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto,Ummy mwalimu amesema Benki ya NMB katika kipindi hiki cha serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha na kuendeleza elimu ya fedha katika ngazi zote hususan katika wanajamii Wa Tanzania.

Hayo ameyaeleza Wakati akizindua rasmi kampeni ya kutoa elimu ya fedha kwa watoto, wazazi na vijana hapa nchini inayoendeshwa na NMB.

Wakati huohuo Naye Mkurugenzi Mtendaji Wa NMB, Ineke Bussemaker alisema Benki yao imejidhatiti kutoa elimu kwa watoto na wazazi kama sehemu yao ya kuendelea na kuimarisha Benki hiyo kwani imekuwa ikiwajali wananchi wake na hasa kuwawekea akiba watoto pindi wanapohitaji kwa matumizi ya baadae hususani katika elimu zao.

You may also like