Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Hospitali ya Taifa Muhimbili itashirikiana na Chuo Kikuu cha Tiba kilichopo Bayreuth nchini Ujerumani katika kuwajengea uwezo wataalamu wa Kitengo cha Upasuaji Rekebishi wa MNH(reconstructive surgery).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi alipokutana na ujumbe kutoka katika chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Prof. Janabi amesema kuwa eneo la upasuaji rekebishi limesahaulika sana kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakati wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ni wengi.

“Wataalamu wakijengewa uwezo wanaweza kufanya upasuaji huu wenyewe na kuwafundisha wengine jambo litakalosaidia wananchi wengi wanaohitaji huduma hiyo” amesema Prof. Janabi.

Prof. Janabi ameagiza hati ya mashirikiano (MoU) iandaliwe haraka ili utekelezaji uanze.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Upasuaji Rekebishi kutoka Chuo Kikuu Tiba cha Bayreuth Prof. Juergen Dolderer amesema tayari taasisi yake inafanya kazi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) na kwamba sasa inapenda kushiriakina na MNH ili kuboresha zaidi huduma hizo.

By Jamhuri