Uchaguzi huu unaonekana kuwa kinyang’anyiro kikali kati ya wagombeaji Bw Odinga na Bw Ruto.

Bw Odinga kiongozi wa upinzani wa muda mrefu, anayeitwa Baba “baba” na wafuasi wake, anawania urais kwa mara ya tano. Bw Ruto, ambaye amejaribu kusisitiza uhusiano wake na Wakenya wa kawaida kwa kujiita “hustler”, atakuwa akiwania kwa mara ya kwanza kwenye kiti cha urais.

Wagombea wengine wawili – David Mwaure na George Wajackoya – pia wako kwenye kinyang’anyiro hicho.

Licha ya kampeni kutawaliwa na masuala ya uaminifu wa kikabila pia unaweza kuchukua sehemu katika kuamua jinsi watu wanavyopiga kura.

Kwa mara ya kwanza katika enzi ya vyama vingi hakuna mgombeaji mkuu anayetoka katika kabila kubwa zaidi nchini – Kikuyu.

Lakini wakijua kwamba kura hizo ni muhimu, wote wamechagua wagombea wenza wa Kikuyu.

By Jamhuri