Vanessa Mdee shinda Tuzo Ya ‘Nyota Wa Mchezo’

Mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy akimkabidhi Tuzo ya ‘Nyota Wa Mchezo’, Mwanamuziki, Vanessa Mdee maarufu Vee Money.

Vanessa Mdee amekuwa msanii wa kwanza Tanzania kupokea Plaque ya ‘Nyota Wa Mchezo’ baada ya kutajwa kama ‘Nyota wa Mchezo’ kwenye vipengele vya BestFemaleAct, BestPerformer, BestLiveAct #EmergingArtistOfTheYear.
Plaque hiyo inatolewa na kipindi cha The Playlist cha Times FM na mtangazaji Omary Tambwe aka Lil Ommykwa kutambua mchango na mafanikio ya msanii na kazi nzuri aliyozofanya.
Kwa mujibu wa Lil Ommy, lengo la Plaque hiyo ni kuwapa nguvu na kusherehekea mafanikio ya kazi za msanii na sanaa kwa ujumla Tanzania.
“Wazo la kumtambua na kumtunuku ‘Nyota wa Mchezo’ lilianza Disemba mwaka jana tarehe 18 ambapo nilitumia twitter kutaja wasanii wengi kama ‘Nyota wa Mchezo’ kuwatambua waliofanya vizuri kwenye sanaa ya muziki wa kizazi kipya,” amesema Lil Ommy.
“Vanessa alikuwa ni miongoni mwa mtu wa kwanza kuandika tweet yake na wazo lilianzia baada ya kumfikiria yeye na kuona kazi nzuri alizofanya na baadae nikaendeleza orodha ya watu wengi kwa hashtag ya #BongoFleva2017 #NyotawaMchezo na kutaja nafasi zao (vipengele) ambavyo wamefanya vizuri,” ameongeza.