Droo ya hatua ya pili ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam imefanyika hii leo ambapo vigogo wa ligi kuu Tanzania Bara wameingizwa katika ratiba hiyo baada ya kutohushishwa katika hatua ya kwanza.  

Simba SC watakutana uso kwa uso na Eagle FC wakati Azam wakikutana na Malimao FC, Yanga watavaana na Kurugenzi FC na Singida Big Stars watakutana na Lipuli FC katika hatua ya pili ya Michuano ya ASFC hatua ya pili ambayo itahusisha timu 64. 

Zinazohusiana

– Bocco aivuruga Simba

 Simba yanyakua pointi tatu kwa Polisi

Timu za ligi kuu zimepangiwa wapinzani wao kama ifuatavyo:

Mtibwa Sugar vs TRA Kilimanjaro

Tanzania Prisons vs Misitu, Coastal Union vs Tanga Middle, KMC vs Tunduru Korosho, Geita Gold vs Transit Camp, Ihefu vs Mtama Boys, Kagera Sugar vs Buhare, Dodoma Jiji vs TMA Stars, Ruvu Shooting vs Ndanda FC, Namungo vs Kitayose, Polisi Tanzania vs Nyika, na Mbeya City vs Stand FC

Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Desema 9 mwaka huu ili kuweza kupata timu ambazo zitafuzu katika hatua ya 32 Bora ya Michuano hiyo.