Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wamewasilia katika Ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuitikia mwito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya viongozi waliowasili ni pamoja na wenyeviti,makamu wenyeviti na makatibu wakuu na katika mkutano unatarajiwa kujadiliwa masuala mbalimbali ya kisiasa nchini ikiwa ni muelekeo mpya wa Rais Samia katika kuboresha siasa za Tanzania.

Waliowasili ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa UDP John Cheyo, Mwenyekiti wa ADC Hamad Rashid Mohamed, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Juma Duni Haji,Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe.

Kabla ya mkutano wa leo kati ya Rais Dk.Samia na viongozi wa vyama vya siasa, tayari kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi wa vyama hivyo na kujadiliana masuala mbalimbali huku akiunda tume maalumu ambayo inayoratibu masuala ya kisiasa nchini na miongoni mwa mambo yanayopewa nafasi kubwa kujadiliwa ni kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.

Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Juma Khatibu (kulia), akizungumza na viongozi waliofika Ikulu leo Januari 3,2023 kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya viongozi wa vyama siasa wakiwasilini Ikulu Dar es Salaam leo Januari 3, 2023
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC) Doyo Hassan leo Januari 3,2023 Ikulu Dar es Salaam.Mpigapicha wetu

By Jamhuri