Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani Msuya, aliyemteua tarehe 03 Januari, 2023 kuwa Katibu Mkuu Ikulu.


Aidha, Rais Samia amemteua Bw. Mululi Majula Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Bw. Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.

Mnamo tarehe 3, Januari Rais Samia alimteua Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

By Jamhuri