Na Tatu Saadi, JAMHURI

Washiriki pekee wa ligi ya klabu bingwa Afrika kutoka Tanzania  Simba Sc, wameendelea kutembeza kipigo kwa Vipers kwa kuwafunga tena Leo katika uwanja wa mkapa jijini Dar es salaam.

Simba Sc wameibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao kutoka Uganda Vipers , na kuongeza alama tatu ambazo zimewasaidia kufikisha alama sita katika msimamo wa kundi Lao.

Huu ni mchezo wa marudiano kati ya Simba na Vipers wakitimiza jumla ya mechi nne tangu hatua ya makundi kuanza ambapo SIMBA na Vipers wanashiriki katika kundi C.

Bao la SIMBA lilifungwa kwenye dakika ya kwanza ya nyongeza ya kipindi cha kwanza, bao pekee lililofungwa na Clatous Chama.

Awali simba Sc ilimchapa Vipers 1-0 katika Uwanja wa nyumbani wa vipers ‘St Mary’s  stadium huko nchini Uganda, bao lililofungwa na beki wa Klabu hiyo, Henock Inonga.

Simba sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi C ambalo lina jumla ya timu nne, wakiongozwa  na Raja Casablanca mwenye alama 12, huku Horoya Ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama  nne na Vipers inaburuza mkia kwa alama moja.

By Jamhuri