Na Tatu Saad, JAMHURI

Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limeweka hadharani zawadi kwa Bingwa wa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kombe la shirikisho msimu huu 2022/23.

Zawadi kwa Bingwa wa Michuano hiyo imewekwa wazi, huku Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikiwa katika hatua ya Makundi Mzunguuko wanne ambao rasmi ulianza kuchezwa jana.Jumanne (Machi 07) katika viwanja mbalimbali Barani humo.

CAF imeeleza kuwa Bingwa wa michuano hiyo atanyakuwa kiasi cha Dola za Marekani Milion 2.5 ambayo ni sawa na takribani 5,830,125,000,000 za Kitanzania na mshindi wa pili kupata Dola 1.25 ambayo ni sawa na 2,915,063,500,000 za Kitanzania.

Na kwa upande wa timu zitakazofika hatua ya Nusu fainali zitapatiwa Dola za Kimarekani 800,000 sawa na 1,865,640,000 za Kitanzania wakati timu zitakazofuzu hatua ya robo fainali zitapatiwa kiasi cha Dola 650,000 sawa na 1,515,832,500 za Kitanzania.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika Bingwa atazawadiwa Dola za Marekani Milioni 1.25 sawa  na shilingi 2,915,062,500,000 za Kitanzania huku Mshindi wa pili atachukua Dola za Marekani 625,000 ambazo ni sawa na Shilingi 1,457,531,250 za Kitanzania.

Na kwa watakaofika Nusu Fainali watapatiwa Dola za Marekani 450,000 sawa na Shilingi 1,049,422,500 za Kitanzania huku watakaofika robo fainali Watapatiwa Dola za Marekani 350,000, sawa na Shilingi 816,217,500 za Kitanzania, nafasi ya tatu na nne hatua ya makundi Dola za Marekani 275,000 sawa na Shilingi 641,313,750 za Kitanzania.

Simba na Yanga Ndio timu pekee kutoka Tanzania zinazoshirki michuano hiyo, SIMBA wakishiriki LIGI Ya mabingwa Afrika huku Yanga wakishiriki kombe la shirikisho na wote wanapambana katika makundi yao ili kuiona hatua inayofuata (robo fainali)