Na Mwandishi wetu, JAMHURI

Mshambuliaji na nahodha wa timu Vipers ya Uganda amesema yupo tayari kucheza soka la Bongo kwani lina muamko na ushawishi mkubwa.

Mshambuliaji huyo ambaye ni muhimu katika kikosi cha Vipers amesema soka la bongo linaopendwa na mashabiki zake (watanzania) tofauti na Uganda, ambako muamko unazidi kuyoyoma kila siku hadi inapelekea kupoteza hadhi ya ligi kutokana na ukosefu wa ushindani katika ligi.

“Napenda sana soka la Tanzania. Mashabiki wa huku wanapenda sana mpira. Wewe ulikuja Uganda na ukaona jinsi ilivyokuwa, huku mashabiki wana muamko zaidi na soka”Alisema Karisa.

Aidha Karisa alisema kila mchezaji ana ndoto ya kucheza sehemu yenye muamko wa mashabiki kama Tanzania hasa pale timu inapokuja na ofa nzuri mezani kwasababu pia wanacheza soka ili kutengeneza pesa.

“Ni ndoto ya kila mchezaji kucheza sehemu yenye muamko wa mashabiki kama hapa Tanzania lakini zaidi ikija ofa nzuri mezani tutafanya kazi kwasababu tunahitaji kutengeneza pesa pia” Amesema Karisa.

Karisa hakuongozana na kikosi cha Vipers kilichocheza dhidi ya Simba Sc jana kutokana na majeruhi aliyoyapata katika mchezo wa awali dhidi ya Simba sc uliopigwa huko Uganda ambapo Karisa alipata majeraha kipindi cha kwanza na kushindwa kuendelea na mchezo.