Na Tatu Saad, JAMHURI

Kocha mkuu wa Klabu ya Al hilal ya nchini Sudan, Florent Ibenge ameanza kuwashawishi viongozi wa klabu hiyo kufanya mchakato wa kupata saini ya Beki muhimu wa klabu ya Simba Sc, Henock Inonga raia wa Congo.

Ibenge amempendekeza Inonga ili kukiboresha kikosi chake hasa kwa upande wa ulinzi kwani Ndio sehemu ya kwanza aliyoiona inahitaji uboreshwaji.

Licha ya kuwa na wakati mzuri katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu lakini Ibenge ameona kuna haja kubwa ya kupata huduma ya Inonga.

Kwa upande wa Simba Sc kupitia Afisa  habari wake Ahmed Ally amesema wao kama timu hawawezi kumzuia mchezaji yoyote akitaka kuondoka.

 “Kama uongozi hatumzuii mchezaji yeyote kuondoka hapa Simba, kikubwa taratibu zifuatwe za usajili.” amesema Ahmed.

Henock ni mchezaji muhimu na tegemezi kwa timu ya simba hasa katika safu ya Ulinzi, amekuwa akiwapa huduma nzuri SIimba sc tangu ajiunge nao.