Kimbembe cha michuano ya Kombe la Dunia hatua ya 16 bora kinaendelea leo kwa mechi mbili kushika kasi huko Urusi.

Kunako majira ya saa 11 jioni, Urafansa itakuwa inacheza dhidi ya Argentina, mechi ambayo itakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na timu hizo mbili kuzungukwa na nyota wawili wakubwa.

Ufaransa watakuwa wanaingia dimbani wakiwa na nyota wao anayekipiga Atletico de Madrid ya Spain, Antoine Griezmann huku Argentina wakiwa na nyota wao, Lionel Messi kutoka FC. Barcelona.

Na baada ya kibarua hicho, baadaye majira ya saa 3 usiku, Ureno nao wakiongozwa na Cristiano Ronaldo watakuwa kibaruani kucheza dhidi ya Uruguay ambayo itakuwa na nyota kadha wa kadha akiwemo Luis Suarez kutoka Barcelona.

Kumbuka mechi hizi zinaoneshwa mubashara kupitia kituo chako cha Star Times, fanya kulipia king’amuzi chako uweze kushuhudia.