ALIYEKUWA mpenzi wa Diamond Platinumz, Zarina Hassan “Zari The Bosslady”, amefunguka kuhusu alivyoombwa msamaha mara kibao na watu mbalimbali akiwemo Babu Tale ambaye hivi karibuni alisafiri hadi Afrika Kusini kumshawishi arudiane na staa huyo.

 

“Babu Tale alikuja Pretoria, alitaka turudiane na Diamond kwa ajili ya watoto, sikuona ubaya katika hilo, lakini mambo ya mapenzi hapana tena, watu haohao wa karibu walipaswa kumuonya Diamond wakati anafanya mambo yake kwa sababu anaamini walifahamu kila kitu.

 

“Wangemwambia Diamond aache mambo aliyokuwa anayafanya. Kufufua penzi kwa sasa ni vigumu sana, wameshachelewa. Mimi nawaheshimu sana, na ndiyo maana hata Babu Tale alipokuja nilimkaribisha vizuri. Sina ubaya na mtu yeyote, hata ndugu zake Diamond,” alisema Zari.

 

Kuhusu Picha na Watoto

“Diamond alikuja kuwaona wanawe. Alilala chumba kingine na mimi nikalala chumbani kwangu. Tuliongea kuhusu kuwa karibu lakini ni kwa ajili ya watoto tu. Kwa sasa sina uhusiano wowote.  Nimeyaweka kando mambo hayo, nachoangalia ni kulea watoto wangu,” alifunguka Zari.

 

Anafunguka Kuhusu maisha yake binafsi.

“Kuna watu wengi sana hawajui maisha halisi ya Zari, wanakisia tu mitandaoni, Ninaandaa shoo yangu ya TV, ambayo inazungumzia maisha yangu halisi, nadhani wengi watamjua Zari halisi. Nina mambo mengi wasiyoyajua.

 

“Hawajui hapa Afrika Kusini nimewekeza kiasi gani? Ivan aliacha mali kiasi gani? Haya natakiwa kuyaendeleza kwa ajili ya watoto wake. Yapo magari yake ya kifahari hata mimi siyaendeshi. Kuna mtoto wake mmoja atatimiza miaka 17 mwakani, ataruhusiwa kupata leseni na ataendesha.”

 

“Tuna shule hapa Afrika Kusini, kampuni ya ulinzi, nimeajiri wafanyakai 360, kila mwisho wa mwezi nalipa mishahara yao. Siwezi kujibizana na mtu mitandaoni”alisema Zari.