Na Patrick Mabula , Shinyanga
Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu wapatao sita wamefariki dunia na wengine 11 kunusurika baada ya kufikiwa na kifusi kwenye machimbo ya dhahabu ya Mwakitolyo , halmashauri ya Shinyanga.
Watu hao walifukiwa katika machimbo ya Mwakitolyo namba 2 kitalu namba nane yaliyonamuwekezaji wa Kichina mei 17 saa tano asubuhi walipokuwa wakifanya shughuli yao ya uchimbaji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga , Anamringi Macha akiongea katika eneo la machimbo hayo alipokwenda kujionea tukio hilo na kuwapa pole alisema wachimbaji hao walifukiwa mida ya saa tano asubuhi na uokoaji ulianza mara moja.
Macha alisema katika uokoaji huo watu sita walikuwa wamefariki na majeruhi 11 waliokolewa na kukimbizwa katika hospitari ya rufaa ya Mwawaza halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa matibabu.

Alisema serikali imepokea taarifa za ajali hiyo kwa masikitiko makubwa na inatoa pole kwa waliopoteza ndungu zao na kuwashukuru wote waliojitoa katika kuwaokoa waliokuwa wamefukiwa na wataona namna ya kuwasaidia waliopatwa na janga.
Macha alitoa wito kwa wachimbaji wa dhahabu kufanya kazi kwa kuzingatia usalama wa kazi yao kwa kufaata taratibu , kanuni na sheria za uchimbaji ili kuepukana na ajali katika maeneo yao ya kazi zao.
Awali wachimbaji hao Emmanuel Joseph,George Chacha juu ya tukio wakiongea mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama walisema wenzao wakiwa katika shughuli zao ghafla kipande cha ardhi kimeguka na kuwafukia.
Joseph alisema kutokea kwa ajali hiyo walianza kupiga yowe na kuwatoa taarifa kwa wenye reseni na wawekezaji walianza kushirikiana kuwaokoa wenzao na kufanikiwa kuwakuta majeruhi 11 na sita wakiwa wamepoteza maisha.