Balozi wa Iran nchini Tanzania, Hossein Alvandi akipiga kura.

Na Dk Mohsen Maarefi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

WAIRAN wanaoishi nchini wamepiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa rais mpya kwa kuhudhuria ubalozi wa Iran jijini Dar es Salaam.

Uchaguzi huo wa muhula wa 14 wa urais wa Iran ulifanyika nchini Iran jana, Juni 28 kwa ajili ya kuchukua nafasi ya rais marehemu Ebrahim Raisi.

Uchaguzi huo ulifanyika kwa wakati mmoja na Iran katika nchi mbalimbali na Tanzania, ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Dar es Salaam uliandaa uchaguzi kwa Wairani wanaoishi Tanzania kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Dkt. Mohsen Maarefi Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran, Mshauri wa kitamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,
Dar es Salaam, Tanzania.

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Tanzania, Hossein Alvandi akiwashukuru Wairani wanaoishi Tanzania waliofika ubalozini kushiriki katika uchaguzi wa rais, alisema kupiga kura kwa Wairani kama wajibu wa kitaifa na hisia ya kujitolea kwa nchi yao na kushiriki katika maendeleo ya taifa.

Rais marehemu wa Iran, Ebrahim Raisi, alifariki Mei 19 mwaka huu, katika ajali ya helikopta iliyokuwa ikimbeba.

Kwa mujibu wa Katiba ya Iran, katika tukio la kifo cha rais, makamu wa kwanza wa rais anachukua madaraka na majukumu kwa muda mfupi na anatakiwa kuhakikisha kwamba ndani ya muda usiozidi siku hamsini, uchaguzi wa rais mpya unafanyika.

Katika uchaguzi huu wa Iran, makamu wa kwanza wa rais marehemu hakugombea na uchaguzi ulihusisha wagombea wanne kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa.

Katika uchaguzi huo kuna wagombea wanne, wakiwemo Mohammad Bagher Ghalibaf na Saeed Jalili, Mwanamageuzi, Masoud Pezeshkian na mwenye msimamo wa kati Mostafa Poormohammadi.

Mgombea anahitaji kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura ili kushinda moja, duru ya pili kati ya wagombea wawili wa juu itafanyika wiki ijayo.