Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia

Wakazi wa kijiji cha Pande plot wilayani Kilwa mkoani Lindi wamelalamika kutolipwa pesa za korosho za msimu uliopita.

Akizungumza na JAMHURI DIGITAL kwa niaba ya wenzake Said Danga amesema,hawajalipwa malipo ya korosho na hawana tarifa zozote mpaka sasa.

Amesema kuwa kero nyingine ni kuwepo kwa gharama kubwa za kulihudumia zao hilo huku kipato na makato yake ni makubwa pamoja na usafiri.

Amesema wamekuwa wakilipishwa sh.6000 kwa gunia kwenda kwenye ghara kutoka na usafiri kuwa shida na barabara ni mbovu .

“Kwa sasa tumevunjika moyo tumeacha kupalilia na tumeelekeza nguvu zetu katika masuala mengine kama kilimo cha ufuta na mwani “amesema.

Amesema wanalima ufuta na mwani kwa sababu ndio mazao makubwa, yasiyokuwana na tozo kubwa kwa sababu mkulima akilima korosho bei ni sh.1700 na tozo sh.360 wakati ufuta sh.1200 na makato sh 130.

Danga amesema changamoto nyingine ni tozo ya unyaufu zimekuwa kero katika zao hilo,kwa sababu hakuna uwazi wa zoezi hilo na watu wamekuwa wakidhulumiwa.

Mkulima Mohamedi Issa amesema kumekuwa na kero ya bwana shamba ambaye amekuwa hana vikao na wakulima na hawaelekezi namna ya kulima kisasa.

Naye Mariam Selemani amesema kuwa Serikali kwa sababu wamekuwa wakitumia sh.milioni moja kwa ajili ya pembejeo kwenye mavuno wanapata sh 500,000

Mariamu amesema changamoto nyingine ni changamoto ya usafiri wa majini ambapo wamekuwa wakivuka katika mitumbwi ambayo sio salama na hasa nyakati za mvua.

Akijibu changamoto hizo Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Christopher Ngubiagai, amekiri kuwepo kwa changamoto hizo ambapo tayari wameshaanza kuzifanyia kazi.

Amesema suala hilo lilipokuja lilikuwa nje ya uwezo wao kwa sababu ,benki waliyokuwa wakitumia wakulima hao kupokelea malipo yao ni ilikuwa ni YETU BENKI ambapo taasisi hiyo imeshafirisika.

“Sasa Sutokana na changamoto hiyo serikali baada ya kuona hivyo ikabeba dhamana kuwalipa malipo yao kupitia Benki ya NMB tayari utaratibu unaendelea wanatakiwa wafungue akaunti mpya ili waweze kulipwa pesa zao.