Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesema changamoto zilizopo kwa sasa ni ndogo kulinganisha na kipindi Rais Ali Hassan Mwinyi aliposhika madaraka.

Akizungumza wakati wa kuuaga mwili wa kiongozi huyo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Warioba amesema kipindi Mwinyi anaingia madarakani hali ilikuwa mbaya sana.

“Tuna matatizo tuna upungufu wa sukari, matatizo ya umeme, tuna matatizo ya maji lakini matatizo tuliyonayo sasa hivi ni madogo sana ukilinganisha na wakati mzee Mwinyi aliposhika uongozi,” amesema Warioba.

Warioba amesema kipindi cha Mwinyi nchi ilikuwa na upungufu wa mafuta, pia alikuta nchi haina bidhaa mbalimbali na kulikuwa na upungufu wa chakula, ila aliunda timu ya kumsaidia kupambana na changamoto hizo.

By Jamhuri