Watakaosalimisha silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kusamehewa

Jeshi la Polisi linapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa,kutakuwa na uzinduzi wa kampeni maalum ya mwezi mmoja unaojulikana kama msamaha wa Afrika itakayohusisha usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari zinazomilikiwa na baadhi ya watu kinyume cha sheria, ama kwa kutokujua taratibu za kisheria za umiliki wa silaha.

Akitoa taarifa hiyo leo septemba 03 2022 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP-Davidi Misime amesema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Septemba 5,2022 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika viwanja vya Mashujaa mkoa Dodoma,ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (MB).

Aidha Misime amesema baada ya uzinduzi huo tushirikiane sote kuelimishana wananchi kuwa yeyote atakayesalimisha silaha anayo miliki kinyume cha sheria katika muda utakaotolewa na Waziri siku hiyo, hatochukuliwa hatua yeyote ile.