Watatu wafariki ajali ya Precision Air

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Issessanda Kaniki ameeleza kuwa kumetokea vifo vya watu watatu katika ajali ya ndege ya Precision Air Bukoba mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu, wawili kati ya hao waliofariki ni wanaume na mmoja ni mwanamke huku akiongeza kuwa juhudi za uokozi na msaada kwa majeruhi zinaendelea.

Ndege hiyo imeanguka leo asubuhi mjini Bukoba wakati ikitua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Askari wa Zimamoto na uokoaji pamoja na Polisi na wavuvi wa eneo hilo wako kwenye eneo la tukio wakifanya shughuli ya uokoaji.