Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mbeya


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewahukumu Afisa Mtendaji wa Kata ya Iwindi na wenzake wawili kulipa faini ya Shilingi 500,000 kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kupokea rushwa kiasi cha sh. 130,000 kinyume na kifungu cha 15(1)(a) na (2) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007.

Hukumu hiyo dhidi ya Bw Rubaha Mkwekwele Sonje, Bw Alex lauden Chawe na Bi Lenisa Raphael Simon katika shauri la jinai Na. 09/2023, ilitolewa Juni 10, 2024 na Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya. Mhe. Scout Peter Andrew.

Washtakiwa walifikishwa kizimbani kwa shtaka la kupokea rushwa kiasi cha sh. 130,00 toka kwa mwananchi ili waweze kumpatia barua ya utambulisho wa kumdhamini ndugu yake aliyekuwa anashikiliwa kituo cha polisi Mbalizi.

Washtakiwa wamelipa faini na kuachiwa huru.