Watu 54 wameuwawa wakiwa sokoni mjini Omdurman baada ya shambulio lililofanywa na wanamgambo wa RSF siku ya Jumamosi.

Kulingana na wahudumu wa afya ambao wameomba kutokutajwa majina kwa sababu za kiusalama, majeruhi wa tukio hilo bado walikuwa wakiendelea kufikishwa katika hospitali ya Al Nano.

Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo walisema shambulio lilitokea magharibi mwa Omdurman kunakodhibitiwa na wanamgambo wa RSF . Tukio hilo limejiri siku kadhaa tangu kiongozi wa wanamgambo hao Mohamed Hamdan Daglo kuapa kuwa atalifurusha jeshi katika mji mkuu Khartoum.

Tangu mwezi Aprili mwaka 2023, kundi la RSF limekuwa likipambana na jeshi rasmi la Sudan, katika mzozo mbaya zaidi ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kupelekea wengine zaidi ya milioni 12 kuyakimbia makazi yao.