ZAIDI ya watu 90 wamefariki dunia baada ya boti yao kupinduka

Mamlaka nchini humo zilisema wasafiri hao walikuwa wakikimbia mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu na walikuwa wakitoka Lunga kuelekea Kisiwa cha Msumbiji, kando kidogo ya pwani ya Nampula.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko, mashua hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukuwa watu 100, lakini wakati inazama ilikuwa imepakia watu wapatao 130.

Shirika la habari la AIM liliripoti kuwa chombo hicho kilipigwa na dharuba kali wakati kikiwa katikati ya mkondo.

Msumbijiinakabiliwa hivi sasa na mripuko mkubwa kabisa wa kipindupindu, ambao haujawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya robo karne, kwa mujibu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).

Tangu mripuko huo uanze mwezi Septemba 2022, zaidi ya watu 37,000 wameshaambukizwa.

By Jamhuri