Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana ameongoza maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wa Arusha kuaga na kutoa heshima ya mwisho kwa Miili ya marehemu waliofariki katika ajali mbaya iliyohusisha lori na magari madogo matatu katika eneo la Ngaramtoni nje kidogo ya jiji la Arusha katika barabara kuu ya Arusha – Namanga

Miili ya marehemu 11 pekee kati ya 25 waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita ndiyo iliyoagwa huku miili 14 ikiwa imeshachukuliwa na ndugu zao.

Balozi Dkt.Pindi Chana amewasilisha salamu za pole za serikali huku Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella akitoa taarifa za maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwafariji wafiwa kwa kushiriki kikamilifu katika mazishi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Loy Thomas Ole Sabaya amewasilisha salamu za Katibu Mkuu wa chama hicho Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.

Please follow and like us:
Pin Share