Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI ,SELELAM JAFO amesema i WAKALA WA MAJENGO TANZANIA –TBA  umekuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya Serikali.

Ametoa kauli hiyo wilayani IKUNGI mkoani SINGIDA baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na wakala huyo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisusua licha ya serikali kulipa gharama za utekelezaji wa miradi hiyo ya ujenzi wa majengo ya serikali;

Katika ziara yake aliyofanya wilayani IKUNGI ,waziri huyo pia alitembelea miradi ya maji ambapo alionyesha kutoridhika na utekelezaji wa baadhi ya miradi  ya maji.

Ziara hiyo ikamfikisha hadi katika makao makuu ya wilaya ya IKUNGI ambapo alikagua ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali   na nyumba za  watumishi wa serikali zinazojengwa na TBA

Akiwa hapo Katibu tawala wa Mkoa wa SINGIDA, ANGELINA RUTAMBI na Mkuu wa wilaya ya IKUNGI MIRAJI MTATURU wakaonyesha kutoridhika na utendaji wa kazi wa TBA kwani licha ya kulipwa fedha bado imeshindwa kumaliza ujenzi wa majengo waliyoakabidhiwa

Please follow and like us:
Pin Share