na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amezitaka taasisi za elimu nchini kuongeza kasi ya upandaji miti kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Jafo ametoa wito wakati akihutubia kwenye mahafali ya kwanza ya lidato cha sita ya Shule ya Fountain Gate Dodoma, Aprili 20, 2024 ambapo ameonesha kuridhishwa na namna wanafunzi wa shule hiyo
wanavyojikita katika elimu ya mazingira.

Amesema mabadiliko ya tabianchi ni ajenda ambayo athari zake ni kubwa zinazosababisha mvua zisinyeshe kwa wakati au kunyesha kwa kiwango kisichotarajiwa hali inayosababisha mafuriko.

Halikadhalika, Dkt. Jafo ametanabahisha kuwa mabadiliko ya tabianchi husababisha baadhi ya maeneo kukabiliwa na ukame uliopitiliza na hivyo kuchangia wanyama kufa na mazao kukauka.

Amesema kutokana na changamoto hiyo, Serikali kupitia Ofisi ya
Makamu wa Rais Januari 20, 2022 ilizindua mpeni ya ‘Soma na Mti‘ inayomtaka kila mwanafunzi wa shule ya msingi, sekondari na chuo kupanda mti.

“Nimefurahi sana kusikia vijana hapa shuleni wakati wa risala yao wanazungumza ajenda ya mabadiliko ya tabianchi, hii maana yake sasa tutakuwa na taifa la vijana ambalo linajua athari za mabadiliko ya
tabianchi,“ amesema.

Kwa upande mwingine, Waziri Dkt. Jafo amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wanaotaka kuwekeza katika elimu kwa ajili ya kuandaa vijana kusomea fani mbalimbali katika vyuo na hatimaye
walitumike taifa.

………………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akiwasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Fountain Gate Dodoma Aprili 20, 2024 ambapo alikuwa mgeni rasmi
katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akikagua maonesho ya wanafunzi alipowasili katika
viwanja vya Shule ya Sekondari ya Fountain Gate Dodoma Aprili 20,
2024 ambapo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya kidato
cha sita.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akiwa na viongozi na baadhi ya walimu wa Shule ya
Sekondari ya Fountain Gate Dodoma Aprili 20, 2024 ambapo alikuwa
mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akihutubia katika mahafali ya Shule ya Sekondari ya
Fountain Gate Dodoma Aprili 20, 2024 ambapo alikuwa mgeni rasmi
katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato
cha sita wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya
Fountain Gate Dodoma Aprili 20, 2024 ambapo alikuwa mgeni rasmi
katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita

Please follow and like us:
Pin Share