Kiwanja cha mpira wa goli kimeendelea kuwaka moto wakati timu za mchezo huo zikipimana nguvu katika michezo ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika Tabora.

Katika mchezo uliofanyika leo katika Chuo cha Uhazili Tabora, timu ya wavulana ya Mkoa wa Tanga imeiadhibu bila huruma Pwani kwa magoli 16-5 huku wenyeji Tabora wakiutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuiadhibu Rukwa kwa magoli 3-1

Kwa upande wa timu za wasichana Morogoro imeibuka kidedea dhidi ya wenyeji Tabora kwa magoli 13- 1 huku Singida ikiilaza Shinyanga kwa magoli 7-4.

Mchezo wa mpira wa goli unaozikutanisha timu zenye wanafunzi wenye uoni hafifu ni moja ya michezo inayoshindaniwa katika mashindano ya UMISSETA 2024.