Baada ya siku takribani tano kupita tangu kikosi cha Yanga kiweke kambi mjini Morogoro, imeelezwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ameomba mechi moja kukipima kikosi chake.

Taarifa kutoka Morogoro zinasema Zahera ameomba apatiwe timu moja ambayo haishiriki Ligi Kuu Bara ili aweze kukipima vizuri kikosi chake kabla ya kufikia hatua ya kucheza na timu za daraja la juu.

Taarifa zinaeleza Yanga wametuma maombi kwa timu zaidi ya moja mjini humo na ambayo itakubali watakipiga nayo leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi dhidi ya USM Alger.

Ikumbukwe Yanga watakipiga na Alger Agosti 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza, Yanga ililala kwa jumla ya mabao 4-0 jijini Algiers, Algeria ambapo sasa ipo mkiani kunako kundi D ikiwa na alama moja pekee.

Please follow and like us:
Pin Share