Na Isri Mohamed, JamhuriMedia

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Yanga dhidi ya CR Belouizdad, afisa habari wa Yanga, Ali Kamwe ameitangaza siku hiyo kuwa maalum kwa mchezaji Paccome Zouzoua ‘Paccome Day’.

Mchezo huo wa kundi ‘D’  ambao utachezwa Jumamosi Februari 24,2024 utawalazimu mashabiki wa Yanga kupaka ‘Bleach’ kichwani au kwenye ndevu kama ishara ya kumsapoti mchezaji huyo ambaye hupaka bleach kila siku kichwani kwake.

Aidha Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuipa nguvu timu yao ili walipe kisasi baada ya kupoteza mchezo wa awali kwa mabao matatu kwa Nunge.

Mchezo kati ya Yanga vs CR Belouizdad utachezwa Jumamosi katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

By Jamhuri