Na Isri Mohamed

Klabu ya wananchi Yanga leo jioni inatarajia kushuka dimbani dhidi ya Ihefu katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar, saa 1 jioni.

Yanga wanaingia katika mchezo huo wakiwa na mioyo ya kisasi kufuatia matokeo ya mchezo wa awali uliochezwa Oktoba 4, 2023 katika dimba la Highland Estates, Mbarali, Mbeya, ambapo walipoteza pointi tatu kwa mabao mawili kwa moja.

Katika mchezo huo Yanga wanahitaji alama tatu ili kufikisha alama 49 na kuendelea kupigwa na baridi kileleni mwa msimamo wa Ligi, sambamba na kuongeza tofauti ya alama dhidi ya wapinzani wake [Azam na Simba] kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo huku baadhi ya nyota wake wengi waliokosekana kwenye mchezo uliopita wakiwa wamerejea kikosini akiwemo golikipa Diarra, beki Joyce Lomalisa, Kiungo Pacome na washambuliaji kennedy Musonda na joseph Guede.

kwa sasa Ihefu imezidi kuimarika baada ya maingizo mapya yaliyofanyika dirisha dogo la usajili ya mlinda lango Khomeny Aboubakary, Abuya, beki Joash Onyango, Rupia na wengine ambao wote wameingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza.

By Jamhuri