Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetangaza kikosi cha wachezaji 23 cha Timu ya taifa (Taifa Stars) kitakachokwenda Azerbaijan kwa ajili ya michezo ya FIFA Series 2024.

Kikosi hicho ambacho kwa sasa kinanolewa na kocha Hemed Morocco, kimezua mjadala mkubwa baada ya kukosekana kwa beki Dickson Job wa Yanga, Nahodha Mbwana Samatta, Shomari Kapombe na Mzamiru Yassin.

Kwenye safu ya ushambuliaji ambayo wamekoseakana Kapombe na Job, wameitwa Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Lusajo Mwaikenda, Haji Mnoga, Mohamed Hussein, Novatus Dismas, Kennedy Juma na Miano Danilo.

Huku safu ya ishambuliaji wakiitwa na Clement Mzize, Simon Msuva, Kibu Dennis, Abdul Sopu, Ben Strakie na Charles M’mombwa.