Na Isri Mohamed

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta aliomba kutojumuishwa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa.

TFF imesema Samatta alizungumza na Kocha Hemed Suleiman, kabla ya kutajwa kwa kikosi hicho na kuomba asijumuishwe katika safari hiyo ya Azerbaijan kwenye michezo ya FIFA Series 2024, Ombi ambalo limekubaliwa.

Kikosi kitaingia kambini Machi 17, na kuondoka Machi 18, ambapo kitacheza michezo miwili dhidi ya Bulgaria na Mongolla.

Michezo hiyo itachezwa Machi 22 na 25, 2024.