Paccome aitwa timu ya Taifa Ivory Coast

Na Isri Mohamed

Shirikisho la Soka la Ivory Coast limetangaza kumuita kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua kwenye kikosi cha timu yao ya Taifa.

Paccome ameitwa kuchukua nafasi ya kiungo mkabaji wa Nottingham Forest Ibrahim Sangare ambaye amepata majeraha.

Ivory Coast itacheza mechi za kirafiki mbili, dhidi ya Benin Machi 23 na dhidi ya Uruguay Machi 26.

Bado Yanga haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na hali ya mchezaji huyo ambaye aliumia juzi kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Geita Gold.