Na Isri Mohamed, JamhuriMedia

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa watafanya maandalizi bora kupata matokeo chanya.

Ikumbukwe kwamba Yanga kutoka kundi D imetinga hatua ya robo fainali ikiwa na pointi 8 kibindoni vinara wakiwa ni Al Ahly ambao wana pointi 12.

Ni timu mbili kutoka Tanzania zipo hatua ya robo fainali rekodi kubwa Afrika na Tanzania ikiwa inajivunia hilo kwa watani wa jadi Simba na Yanga kutinga kwenye hatua kubwa ya mashindano hayo yanayofuatiliwa na wengi duniani kwenye anga la mpira.

Gamondi amebainisha kuwa kila mashindano yana umuhimu kwa kuwa wapo hatua hiyo Wanakazi kubwa kujipanga katika mechi zote mbili nyumbani na ugenini kuhakikisha kwamba wanapata matokeo mazuri.

“Uzuri ni kwamba tumekuwa na mwendelezo mzuri kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika muhimu kuwa tayari na kujua kwamba haya ni mashindano tofauti na hapa ambapo tupo.

“Uzoefu uliopo pamoja na aina ya wachezaji vinanipa nguvu ya kuamini kwamba kwenye mechi zetu tutafanya vizuri na inawezekana kwani hakuna anayefikiria kutopata matokeo na wachezaji wapo tayari kupambana,”

Kocha Mkuu wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Rhulani Mokwena, anayehusudu zaidi mpira wa pasi nyingi na kufanya maamuzi ya haraka, ameweka wazi kuwa wanafanya maandalizi mazuri kupata ya kujipanga matokeo pia.

“Kuwa kwenye hatua hizi lazima ujiandae kiakili na tutafanya hivyo kwa sababu mashabiki wana matarajio makubwa juu yetu na hatupaswi kuwaangusha kabisa.

“Yanga ni timu nzuri na imetengeneza historia yake kwenye hii michuano ya CAF champions League mfano mwaka jana walifika hadi fainali ya Confederation lakini pia walishinda ligi hivyo ni timu nzuri.”

Mechi za mkondo wa kwanza zinatarajiwa kuchezwa kati ya Machi (29-31) ambapo Yanga na Simba zote zitakuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa na kurudiana kati ya Aprili (5-7), 2024.