Klabu ya Ihefu imevunja rekodi ya Yanga ya kutokufungwa katika mechi ya 50 kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara baada ya kufungwa kwa mabao 2-1, mchezo ambao ulipigwa Mbarali mkoani Mbeya.

Yanga Sc ilianza kupata bao kupitia kwa Yannick Bangala kabla ya Never Tigere kusawazisha kwa kupiga mpira wa adhabu uliomshinda kipa wa Yanga na kutinga nyavuni moja kwa moja.

Bao la pili Ihefu Fc limefungwa na Kissu na kufanya matokeo kuwa 2-1.