Monthly Archives: June 2019

Pongezi kwa wananchi kutii mamlaka

Aprili 9, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alitangaza kwamba kuanzia Juni mosi mwaka huu itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake yatakoma ifikapo Mei 31.  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma kwenye Mkutano wa 15 wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya ...

Read More »

NINA NDOTO (20)

Umri usiwe kikwazo cha kutimiza ndoto   Kuwa na umri fulani si kigezo kuwa huwezi kutimiza ndoto zako. Umri ni namba tu. Bila kujali kama wewe ni mzee au mdogo kiasi gani, bado unaweza kutimiza ndoto zako. Bado unayo nafasi ya kufanya mambo makubwa. Umri usiwe kikwazo cha wewe kutotimiza ndoto zako. Kuna watu wakianza kufikiria kuanza kutimiza ndoto zao ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (16)

Nikiri nimeendelea kupata simu na maswali mengi kuhusu ‘Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania.’ Nimepata simu kutoka Rukwa, Katavi na maeneo ya mbali. Changamoto kubwa ninayoipata ni wahusika kukutana na makala hii katikati bila kusoma za mwanzo. Sitanii, ananipigia mtu anaulizia mambo niliyoyazungumzia katika sehemu ya kwanza, ya pili au ya saba. Inaniwia vigumu pia kuanza kumwelezea mtu mmoja mmoja hatua unazopaswa ...

Read More »

Elimu ni mkombozi wa ulemavu wa fikra

Ulemavu wa fikra umejificha. Wakati mwingine ni vigumu kuutambua au kwa vile ulemavu huu una nguvu na unaweza kutupumbaza wote, ni jambo ambalo linachukua tafakuri na kujiuliza maswali yasiyokuwa na majibu. Mfano, sisi Waafrika kuwa na majina ya Kizungu na Kiarabu au sisi Waafrika kutukuza vizazi vya nchi za nje kuliko kutukuza vizazi vya babu zetu. Au kutukuza na kujivunia ...

Read More »

Umuhimu wa kujenga familia iliyo bora

Mratibu Ofisi ya CPT Taifa, Mariam Kessy, kwenye kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere aliwasilisha mada kuhusu familia. Yafuatayo ni baadhi ya yale aliyozungumza.  Familia kama msingi wa taifa na jamii, kila mmoja anakotoka na anakoishi ni vizuri kuzungumzia familia. Kila tunachofanya lazima kilenge familia. Tunaposema taifa letu ni maskini, maadili katika taifa letu yameporomoka,  ...

Read More »

Ndugu Rais kama si wewe nani atawatoa watoto majalalani?

Ndugu Rais, imeandikwa; kitabu hiki cha Torati kisitoke mdomoni mwako mchana hata usiku. Nami kama Daudi nimetumwa uyatafakari maandiko tuandikayo kwa maana hayo yataifanikisha njia yako kwa kuwa yatakustawisha! Ndugu Rais, kama si wewe baba, ni nani atawatoa jalalani watoto wa Ifakara? Maisha yao ni sawa na yale ya mifugo iliyotelekezwa. Chakula chao wanakipata jalalani baada ya kuchakurachakura kama wafanyavyo ...

Read More »

Kuwapo madini Tanzania ni baraka au laana?

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenijalia kuandika makala hii na kuchapishwa katika gazeti hili mahiri ili kuelimisha na kuwajuza Watanzania nini kinajiri katika sekta ya madini. Tanzania imejaliwa kuwa na rasilimali asilia ikiwemo ardhi, madini, misitu, wanyamapori, maji chumvi/maji baridi, samaki na viumbe hai wengine waishio majini, bioanuai na rasilimali watu. Nilihudhuria mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (UNECA), ...

Read More »

Ukweli japo wa mbaya wako ni ukweli

Siamini yupo binadamu anayekubali kwa hiari kuvumilia ubaguzi wa aina yoyote; kwa hiyo tunaposikia matamshi au kushuhudia vitendo tunavyohisi kuwa vya kibaguzi vinatuamshia mara moja hisia ya kujihami na hata kurejesha mashambulizi. Nilikuwa abiria kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda nikienda kwenye mji wa Kigali nikasikia abiria mwenzangu akisifia usafi na mpangilio mzuri wa jiji hilo. Akaongeza: ...

Read More »

Huwezi kukopa kwa dhamana ya kiwanja, shamba lisiloendelezwa

Wiki iliyopita niliandika kuwa ujenzi wa uzio (fensi) pekee kwenye kiwanja si uendelezaji halisi kwa mujibu wa kanuni mpya za sheria ya ardhi tofauti na tulivyozoea. Leo tena tunatazama sehemu ya (iii) Kanuni ya saba ya kanuni mpya, kanuni za Sheria ya Ardhi kupitia Tangazo la Serikali Namba 345 la Aprili 26, 2019. Kanuni ya 7(1) inasema kuwa mwenye kiwanja/shamba ...

Read More »

Usiamini uwepo wa uchawi

Jamii yoyote ile ni lazima itembee katika ukweli, haki, maadili, mwanga na elimu. Hakuna jamii inayoweza kuendelea pasipo watu wake kuwa wakweli na wenye maadili na akili tafakari na akili bainifu. Hatuwezi kuendelea kutambua kwamba sisi ni wajinga na bado tukaendelea kuishi maisha ya kijinga. Lazima tukubali kubadilika. Tunahitaji kufahamu lipi linaweza kubadilishwa na lipi haliwezekani na zaidi kufahamu tofauti ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (31)

Nyota njema huonekana pia jioni Namna ya kumaliza ni mtihani.  Hoja si namna unavyoanza, hoja ni namna unavyomaliza. “Kuanza vizuri ni jambo la kitambo; kumaliza vizuri ni suala la maisha yote,” alisema Ravi Zacharias – mtunzi wa vitabu. Mwanzo unaweza kuwa mbaya lakini mwisho ukawa mzuri. Lakini kuna uwezekano mwanzo ukawa mzuri na mwisho ukawa mbaya. “Afadhali taabu zianze, za ...

Read More »

Sasa iwe zamu ya ‘chainsaw’

Wiki mbili zilizopita katika safu hii niliandika makala nikieleza hisia zangu kuhusu hatua ya Kenya kutupiku kwenye fursa ya kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Afrika Kusini. Siku chache baadaye, Rais John Magufuli, akawa na ziara katika mataifa matatu – Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe. Kama yapo mambo yaliyowafurahisha Watanzania wengi kwa ziara hiyo, lile la ‘kukieneza’ Kiswahili katika mataifa hayo ...

Read More »

Yah: Kiswahili ni bidhaa ya kuuza nje, walimu changamkeni

Nimeamka nikiwa na furaha sana baada ya kusikia kumbe tunatembea na bidhaa bila kujijua. Ni wachache ambao walikuwa wanajua kwamba Kiswahili ni fedha, hasa ni wale wenzetu  ambao wanatumia mitandao ya kuzunguka duniani wakiwa wamekaa katika viti vyao, sisi huku Kipatimo ni kama tunashangaa, unawezaje kuuza lugha yako unayoitumia? Utabakiwa na nini? Kuna mtu anatangaza hapa Kipatimo kuwa walimu wa ...

Read More »

Tujali Polisi na Mahakama

Ni vema tukakumbuka tuna wajibu wa kujali na kuheshimu (kuthamini) vyombo vyetu vya Polisi na Mahakama, ambavyo tumeviridhia kusimamia usalama wetu na kutoa haki. Ni vyombo nyeti katika mustakabali wa maisha yetu, uhuru na amani ya taifa letu. Polisi katika taratibu zake za kazi ni kusimamia usalama wa raia na mali zao. Inafuatilia kuona kila mtu yupo salama na mali ...

Read More »

Chungeni ndimi zenu

Mtunga Zaburi, Mfalme Daudi aonya hivi: “…Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, jeuri huwavika kama nguo, macho yao hutokeza kwa kunenepa, wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao. Hudhihaki, husimulia mabaya.  Husimulia udhalimu, kana kwamba wako juu.” Zaburi 73:6-8; Mhubiri 8:11, Biblia Takatifu. Wadau ‘wanajamii’ wenzangu; ‘maono’ yaliyonitokea kwa miezi kadhaa yanazidi kunikereketa; niendelee ‘Kusema yaliyo ya kweli na Amani ...

Read More »

Stars chunga hawa!

Ligi mbalimbali duniani zimemalizika katika msimu wa 2018/2019. Fainali ya Europa na UEFA nazo zimemalizika, hicho kikiwa ni kiashiria kwamba wachezaji wanakwenda katika mapumziko na kuanza maandalizi ya msimu mwingine wa ligi. Pazia la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya limefungwa Jumamosi iliyopita kwa fainali baina ya Tottenham na Liverpool. Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Wanda Metropolitano (uwanja wa Atletico Madrid), ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons