Monthly Archives: September 2019

Waziri aharibu

Mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati na Maji (EWURA) umedumu kwa miaka miwili sasa, huku Waziri wa Maji akitajwa kuwa chanzo cha mkwamo huo. Wakati Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, akitajwa kuwa chanzo kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni masilahi yake binafsi, yeye anasema anataka kuona haki inatendeka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ...

Read More »

Ndoto ya JPM ya zimamoto kutengenezwa nchini yatimia

Machi, mwaka huu, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, aliliagiza Shirika la Nyumbu lianze kutengeneza magari ya zimamoto. Hoja ya Rais Magufuli ilikuwa kwamba mpango huo ulenge kupunguza gharama kubwa za ununuzi wa magari hayo kutoka ng’ambo. Siku chache baadaye, alimteua Balozi Luteni Jenerali mstaafu, Wyjones Kisamba, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ...

Read More »

‘Aliyeua’ mkewe mahakamani leo

Mfanyabiashara Khamis Lowongo (Meshack) mwenye umri wa miaka 38 anayetuhumiwa kumuua mke wake, Naomi Marijani, kwa kumchoma moto akitumia magunia mawili ya mkaa Kigamboni, jijini Dar es Salaam amekuwa na vituko mbalimbali kila afikapo mahakamani. Mtuhumiwa huyo kwa mara ya kwanza alikamatwa na Jeshi la Polisi baada ya Gazeti la JAMHURI Julai 16, mwaka huu kuandika habari kuhusiana na uwezekano ...

Read More »

Mimba za utotoni tishio Tarime/Rorya

Mimba za utotoni sasa zimekuwa tishio wilayani Tarime, mkoani Mara. Taarifa rasmi zinaonyesha kwamba katika kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu wanafunzi 51 wanatajwa kupata mimba na kuathiri masomo yao. Akisoma taarifa ya wilaya hiyo, Kaimu Mkurugenzi, Silvanus Gwiboha, amesema kuanzia kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu jumla ya wasichana 51 wamepewa ujauzito na tayari taarifa zao ziko kwenye ...

Read More »

Raia wa Afrika Kusini atupwa jela

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemhukumu Christine Lindiwe ambaye ni raia wa Afrika Kusini kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria. Katika kesi namba 176 ya mwaka 2019, Lindiwe alisomewa shitaka la kuingia nchini kwa njia haramu, ambapo Agosti 14, mwaka huu alikamatwa katika ...

Read More »

Wiki ya huzuni Afrika

Wiki iliyopita yamekuwapo matukio mengi, lakini kwa ngazi ya Bara la Afrika yaliyotawala ni vurugu za xenophobia nchini Afrika Kusini na kifo cha Baba wa Taifa la Zimbabwe, Robert Mugabe. Wageni kadhaa wanaofanya biashara zao nchini Afrika Kusini, hasa katika miji ya Johannesburg na Pretoria, wameuawa na wengine kujeruhiwa kwa kile kinachoonekana ni chuki ya wenyeji dhidi ya wageni. Mali ...

Read More »

NINA‌ ‌NDOTO‌ ‌(34)‌

Niongee lini, ninyamaze lini?   Baada ya kuandika makala yenye kichwa kisemacho: “Ukiwa na ndoto usipige kelele, kaa kimya,” katika Gazeti la JAMHURI, Toleo Na. 411 la Agosti 13-19, 2019 nimepongezwa na wasomaji kwa kunipigia simu wakiniambia kuwa makala hiyo imegusa maisha yao na itawasaidia. Mmoja wao ambaye amekuwa mfuatiliaji mzuri wa makala za ‘Nina Ndoto’ kutoka Arusha aliniuliza swali ...

Read More »

BURIANI ROBERT GABRIEL MUGABE

Mzalendo aliyesalitiwa na jumuiya ya kimataifa Tanzia kuhusu kifo cha mwanamapinduzi nguli wa Afrika, mpigania uhuru wa Zimbabwe na mwana wa Afrika, Robert Gabriel Mugabe, zilianza kusambaa Ijumaa ya Septemba 6, 2019. Salamu za rambirambi zilianza kumiminika kutoka kila kona ya dunia muda mfupi baadaye. Kwa upande wa Tanzania, ambako Mugabe alipachukulia kama nyumbani kwake, Rais Dk. John Magufuli, ambaye ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (28)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii katika sehemu ya 27 kwa kuhoji hivi: “Sitanii, wapo watu wanalipa kodi vizuri, lakini mwisho wa siku wanapata matatizo kwa kutopeleka ushahidi kuwa wamelipa kodi TRA. Je, unafahamu kodi zinalipiwa wapi ikiwamo VAT? Usikose sehemu ya 28 ya makala hii Jumanne ijayo uweze kukomboa biashara yako na uache kufukuzana na TRA. Tunaanzia wanapoishia wengine. Soma ...

Read More »

Nje ya magereza wapo wanaoonewa

Hivi karibuni Rais John Magufuli kwa uwezo aliopewa na Katiba ya nchi aliwasikiliza wafungwa waliomo gerezani Butimba, Mwanza na kubaini kwamba wapo walioonewa na kuwekwa gerezani kwa njia za ukatili tu kama kukomolewa. Akaamuru waondolewe. Hiyo ni hali ya utu ya kuwajali watu aliyonayo rais wetu. Wananchi wanaliona hilo kama njia bora ya kuwajali watu wake, wanapaswa wamshukuru na kumpenda ...

Read More »

UJUMBE KUTOKA IKULU

HOTUBA YA MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA MAZUNGUMZO NA WASHIRIKI WA MKUTANO WA JUKWAA LA UONGOZI AFRIKA, IKULU, DAR ES SALAAM,  TAREHE 30 AGOSTI 2019   Ni heshima kubwa kwangu kupata fursa hii adhimu ya kuzungumza kwenye Mkutano huu muhimu kwa mustakabali wa Bara letu la Afrika. Natambua kuwa huu ...

Read More »

BURIANI KOMREDI IBRAHIM MOHAMED KADUMA

‘Kikitokea chama kama CCM ya Nyerere kitatawala milele’   Mwaka 2012 Gazeti la JAMHURI lilifanya mahojiano maalumu na mzee Ibrahim Kaduma nyumbani kwake Makongo Juu, Dar es Salaam. Tunaleta sehemu ya mahojiano hayo kama tulivyoyachapisha wakati huo. Mzee Kaduma alifariki dunia Agosti 31, 2019 nchini India alikokuwa akitibiwa akiwa na umri wa miaka 82. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage ...

Read More »

Bandari: Usalama wa mizigo 100%

Miaka michache iliyopita, Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa na changamoto ya usalama wa mizigo ya wateja. Mhandisi Deusdedit Kakoko alipoteuliwa Juni 25, 2016 kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), aliahidi kuimarisha ulinzi na kuondoa udokozi bandarini. Mhandisi Kakoko alisema usalama wa mizigo ya wateja unapaswa kuwa namba moja na huo ndio msingi wa Bandari ya Dar ...

Read More »

Wanaiingiza nchi katika machafuko wakisingizia wanakupenda

Ndugu Rais, walituambia kukaa kimya ni kukubali yote; bali kukemea yasiyofaa ndiyo busara na hekima ya kiongozi bora. Watu wako baba wanakupenda kama walivyowapenda marais wengine waliokutangulia. Sasa huu wasiwasi unatokea wapi? Watu wamejaa wasiwasi mwingi katika macho yao. Wasiwasi ni tunda la moyo baada ya mtu kijiridhisha kuwa ametenda uovu mwingi na sasa anachelea kisasi. Hapo wasiwasi huidhoofisha nafsi ...

Read More »

Inahitaji ujasiri wa simba kufichua maovu

Mara kwa mara katika hotuba zake Rais John Magufuli hukumbusha wajibu wa viongozi katika ngazi zote kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia wapiga kura. Amekumbusha tena kwenye hotuba yake hivi karibuni kwa watendaji wa kata aliyowaalika Ikulu. Alisisitiza umuhimu wa watendaji kusimamia utekelezaji miradi ya maendeleo ya Serikali, akiwakumbusha jukumu lao muhimu sana la kudhibiti ubadhirifu na ukiukwaji wa maadili. Alisema ...

Read More »

Ukweli kesi ya Mzungu na Airbus yetu (1)

Kabla ya kukamatwa ndege Mwaka 1983 kupitia Kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act, 1983 kampuni sita za Mzungu Hermanus Steyn ambazo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd, Lente Estate Ltd, Loldebbis Ltd, Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd zilitaifishwa na Serikali ya Tanzania. Baadaye Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi (arbitration) akiomba ...

Read More »

Ukipoteza muda, muda utakupoteza zaidi (3)

Wiki iliyopita, makala hii iliishia pale Marcus Aurelius anaandika: “Kwa sababu jambo linaonekana ni gumu kwako, usifikiri kwa wengine haliwezekani.” Huwezi ukashinda kama huchezi. Neno ‘Haliwezekani’ tulitumie kwa uangalifu mkubwa. Padri Dk. Faustin Kamugisha anaandika: “Kama kila mtu angejitahidi kufanya lolote zuri, dunia ingekuwa mahali pazuri pa kukalika.” “Ushindwe wakati umejaribu.” Ni methali ya Tanzania. Methali ya Sierra Leone inasema: “Usipojaribu hautafanikiwa. ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (45)

Utukufu ni mbele kwa mbele   Yajayo ni mtihani, kioo cha mbele cha gari ni kikubwa kuonyesha kuwa makubwa yako mbele. Vioo vya pembeni vya kutazama ya nyuma ni vidogo kuonyesha kuwa madogo yako nyuma, utukufu ni mbele kwa mbele. “Yajayo ni mazuri zaidi kuliko yaliyopita.” (Methali ya Kiarabu). Jana haiwezi kubadilishwa, lakini kesho ipo ndani ya mikono yako. Usitazame nyuma, ...

Read More »

Kulaza watu saa 5 usiku si haki

Hivi karibuni nilihudhuria sherehe za kijana mmoja aliyefunga ndoa. Ni tukio la furaha kwa wana ndoa wenyewe, lakini pia kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wawili hao. Ni tukio linalowakutanisha watu wengi na huendana na shamrashamra za kila aina. Kula na kunywa pekee havinogeshi sherehe. Sharti kuwepo muziki – uwe ‘live’ au unaotoka kwenye ‘music system’. Tena basi, muziki wenyewe ...

Read More »

Kuna njama za kuhujumu uchumi wetu

Kuna njama za kuhujumu uchumi na kudhulumu utu na uchumi wa Mtanzania daima dumu. Njama hizo si ndogo, ni kubwa na zinatekelezwa usiku na mchana na mabeberu wa dunia wakishirikiana na Watanzania wenzetu. Wananchi hatuna budi kulifahamu hilo na kuwa makini kulishinda. Hivi ninavyozungumza mabeberu na Watanzania hao walioshiba mali ya dhuluma ya mkulima na mfanyakazi katika majiji, miji na ...

Read More »

Yah: Sasa litolewe tamko

Naanza na salamu kama Mtanzania mwenye uzalendo.  Watu wengi hawaelewi maana halisi ya uzalendo. Inawezekana hata mimi nikawa miongoni mwao, kwa maana ya leo ambayo inazungumzwa na wanasiasa wengi vijana na walioibuka katika uwanja wa siasa kama sehemu ya ajira. Kwa ufupi sisi watu wa zamani tulitafsiri uzalendo kama upendo baina yetu kama taifa na upendo kwa taifa letu. Kuna ...

Read More »

Kunahitajika chombo cha kitaifa kuratibu shughuli za Serikali

Awali ya yote nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na wingi wa neema, lakini pia kutupatia uwezo na nguvu kusimamia na kutumia rasilimali zilizopo kwa faida ya kizazi hiki na kijacho. Tanzania imejaliwa kupata rasilimali na vivutio vya kipekee duniani. Kidunia ukitaja hifadhi za Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro au visiwa vya Zanzibar itafahamika unamaanisha Tanzania. Tanzania ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons