Waziri aharibu

Mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati na Maji (EWURA) umedumu kwa miaka miwili sasa, huku Waziri wa Maji akitajwa kuwa chanzo cha mkwamo huo. Wakati Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, akitajwa kuwa chanzo kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni masilahi yake binafsi, yeye anasema anataka kuona haki inatendeka kwa…

Read More

Ndoto ya JPM ya zimamoto kutengenezwa nchini yatimia

Machi, mwaka huu, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, aliliagiza Shirika la Nyumbu lianze kutengeneza magari ya zimamoto. Hoja ya Rais Magufuli ilikuwa kwamba mpango huo ulenge kupunguza gharama kubwa za ununuzi wa magari hayo kutoka ng’ambo. Siku chache baadaye, alimteua Balozi Luteni Jenerali mstaafu, Wyjones Kisamba, kuwa Mwenyekiti…

Read More

‘Aliyeua’ mkewe mahakamani leo

Mfanyabiashara Khamis Lowongo (Meshack) mwenye umri wa miaka 38 anayetuhumiwa kumuua mke wake, Naomi Marijani, kwa kumchoma moto akitumia magunia mawili ya mkaa Kigamboni, jijini Dar es Salaam amekuwa na vituko mbalimbali kila afikapo mahakamani. Mtuhumiwa huyo kwa mara ya kwanza alikamatwa na Jeshi la Polisi baada ya Gazeti la JAMHURI Julai 16, mwaka huu…

Read More

Mimba za utotoni tishio Tarime/Rorya

Mimba za utotoni sasa zimekuwa tishio wilayani Tarime, mkoani Mara. Taarifa rasmi zinaonyesha kwamba katika kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu wanafunzi 51 wanatajwa kupata mimba na kuathiri masomo yao. Akisoma taarifa ya wilaya hiyo, Kaimu Mkurugenzi, Silvanus Gwiboha, amesema kuanzia kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu jumla ya wasichana 51 wamepewa ujauzito na…

Read More

Raia wa Afrika Kusini atupwa jela

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemhukumu Christine Lindiwe ambaye ni raia wa Afrika Kusini kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria. Katika kesi namba 176 ya mwaka 2019, Lindiwe alisomewa shitaka la kuingia nchini kwa njia haramu, ambapo Agosti…

Read More

Wiki ya huzuni Afrika

Wiki iliyopita yamekuwapo matukio mengi, lakini kwa ngazi ya Bara la Afrika yaliyotawala ni vurugu za xenophobia nchini Afrika Kusini na kifo cha Baba wa Taifa la Zimbabwe, Robert Mugabe. Wageni kadhaa wanaofanya biashara zao nchini Afrika Kusini, hasa katika miji ya Johannesburg na Pretoria, wameuawa na wengine kujeruhiwa kwa kile kinachoonekana ni chuki ya…

Read More