Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Umri wa mawaziri umekuwa gumzo kwa nyakati tofauti, wengi wakitamani kuona Baraza la Mawaziri likitawaliwa na vijana.

Na hata wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya mabadiliko mapema mwezi huu, hoja hiyo iliibuka tena.

Ni wakati huo ndipo kwenye mitandao ya kijamii kukasambazwa Baraza la Mawaziri la Tanganyika la mwaka 1963, likionyesha umri wa viongozi wa wakati huo.

Pamoja na kuwa vijana, viongozi hao waliendelea kuwa madarakani hadi wakazeeka huku watu wakihoji, kwa nini hawakuwapisha vijana?

Hili hapa baraza hilo la mawaziri:

Rais: Julius K. Nyerere miaka 41 

Makamu wa Rais: Rashidi Kawawa (34)

Waziri wa Sheria: Sheikh Karuta A. Abedi (39)

Waziri wa Kilimo: Derek N. Maclean Bryceson (40) 

Waziri wa Biashara: Clement George Kahama (34) 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi: Oscar S. Kambona (35)

Waziri wa Mambo ya Ndani: Job Malecela Lusinde (32) 

Waziri wa Mawasiliano: Amir H. Jamal (41)

Waziri wa Fedha: Paul Bomani (38)

Waziri wa Ardhi: Alhaj Said Tewa (37)

Waziri wa Ushirika na Maendeleo ya Jamii: Jeremiah S. Kasambala (38)

Waziri wa Elimu: Solomon N. Eliufoo (42)

Waziri wa Afya: Saidi Ali Maswanya (39)

Waziri wa Kazi: Michael Kamaliza (33)

Waziri wa Serikali za Mitaa: Austine K.E. Shaba (38)

Waziri wa Utamaduni na Vijana: L. Nang’wanda Sijaona (35) 

Waziri wa Mipango na Maendeleo: Nsilo Swai (38).

Katika orodha hii hakukuwapo waziri aliyekuwa na umri wa zaidi ya miaka 42.

754 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!
Show Buttons
Hide Buttons