Gazeti Letu

Ridhiwani matatani

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umemfurusha Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika nyumba ya serikali anayoishi jijini Dodoma, baada ya kushindwa kulipa kodi ya pango, uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umethibitisha. Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kwamba mbunge huyo alishindwa kukamilisha kulipa deni la pango linalofikia takriban Sh milioni 7, hata baada ya muda wa notisi ya siku 14 iliyotolewa na ...

Read More »

Waziri aharibu

Mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati na Maji (EWURA) umedumu kwa miaka miwili sasa, huku Waziri wa Maji akitajwa kuwa chanzo cha mkwamo huo. Wakati Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, akitajwa kuwa chanzo kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni masilahi yake binafsi, yeye anasema anataka kuona haki inatendeka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ...

Read More »

CWT inavyopigwa

Maji yanazidi kuchemka ndani ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT), huku mkataba wa kinyonyaji wa mshauri wa mradi wa ujenzi na madeni kwenye Mfuko wa Jamii wa PSPF, yakiwa ni miongoni mwa mambo yanayoendelea kwenye chama hicho.  JAMHURI limebaini CWT iliingia mkataba wa kinyonyaji na Kampuni ya Settlements De Popolo Consultants wenye gharama ya Sh milioni 960, lakini kutokana na ...

Read More »

Bundi atua wizarani

Baada ya gazeti hili la uchunguzi, JAMHURI, kuandika kuhusu ubovu wa matrekta wanayouziwa wakulima nchini wiki iliyopita, Bunge kupitia Kamati ya Viwanda na Biashara limeingilia kati kunusuru nchi kuingia katika madeni yasiyo na faida, hivyo kumwita Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, ajieleze. Habari za uhakika kutoka bungeni zinaeleza kuwa Jumatano iliyopita uongozi wa Shirika la Maendeleo la Taifa ...

Read More »

Kashfa nzito

Serikali ya Rais John Pombe Magufuli imo hatarini kupoteza zaidi ya Sh bilioni 120 kutokana na mradi wa kukopesha matreka kwa wakulima ambao mkataba uliingiwa siku 8 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kugeuka ‘kichomi’, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Mkataba huo unaotajwa kuwa na mazonge mengi, uliingiwa Oktoba 22, 2015 ikiwa ni wiki moja na siku moja kabla ya ...

Read More »

JWTZ waombwa DRC

Wananchi wa Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameandamana wakitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lipelekwe nchini humo liwakung’ute waasi wanaoua mamia kwa maelfu ya watu. Bado wananchi wengi wa DRC wanatambua na kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na majeshi ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani yaliyoongozwa na JWTZ baada ya kuwafurusha waasi wa March 23 ...

Read More »

Waomboleza

Familia ya Naomi Marijani (36), imefanya maombolezo kwa ibada maalumu baada ya kuthibitika kuwa binti yao ameuawa. Ingawa haijathibitika nani kamuua (kwani kesi ndiyo imeanza), pamoja na mume wake kukiri mbele ya polisi kuwa alimuua na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa nyumbani kwake Gezaulole, Kigamboni, Dar es Salaam na kisha kuzika mabaki shambani kwake Kijiji cha Marogoro, ...

Read More »

Simu ‘yamuua’ Naomi

Siku chache baada ya polisi kutangaza kumkamata Hamis Said Luwongo (38), kwa tuhuma za kumuua na kumchoma moto mke wake, Naomi Marijani, taarifa za kina zimeanza kuvuja na inaonekana simu ya mkononi ilichangia kutokea kwa mauaji hayo. Uchunguzi unaonyesha kuwa miaka mitatu iliyopita, familia ya Hamis na Naomi, iliingia katika majaribu ya hali ya juu baada ya wanandoa hao kutiliana ...

Read More »

Alivyouawa

Siku chache baada ya Polisi kuthibitisha kwamba Naomi Marijani ameuawa, uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba maandalizi ya mauaji yake yalifanyika wiki moja kabla, huku akiishi na mtuhumiwa wa mauaji katika nyumba moja. Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba kulikuwepo na misuguano baina ya Saidi (Meshack) Hamis Luwongo na mkewe, marehemu Naomi Marijani. JAMHURI limethibitishiwa pasi na shaka ...

Read More »

Ameuawa?

Naomi Marijani (36), mama wa mtoto mmoja, mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ametoweka katika mazingira yenye utata kiasi cha kujengeka hisia kuwa ameuawa, JAMHURI linaripoti. Hadi leo zimetimia siku 63 tangu Naomi ametoweka katika mazingira yenye kuacha maswali mengi huku polisi wa Kigamboni wakionekana kutolipa kipaumbele suala la kupotea kwake, japo ushahidi wa mazingira unabainisha wazi mtuhumiwa wa ...

Read More »

Waliomdanganya JPM kibao chageuka rasmi

Miezi miwili tangu aliyestahili tuzo ya mfanyakazi bora wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), James Kunena, kupokwa fursa hiyo saa chache kabla ya kutunukiwa na Rais Dk. John Magufuli katika kilele cha mwaka huu cha Mei Mosi, hali si shwari ndani ya Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Uchunguzi wa JAMHURI umebaini hali ya ‘hasira’ miongoni mwa wafanyakazi wa ...

Read More »

Bomu la ardhi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amepata jaribio kubwa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. “Siku moja baada ya kuingia ofisini, alijifungia ofisini kwake akasema ana shughuli nyingi hivyo asingeweza kumwona mtu yeyote. Ghafla, akaja mzee mmoja. Akamweleza msaidizi wake tukio la kusikitisha. Tukio lenyewe lilikuwa kama sinema vile. ...

Read More »

Mwenyekiti CWT adanganya

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Clement Mswanyama, amewadanganya walimu na Watanzania kwa ujumla juu ya umiliki wa mali za walimu, JAMHURI linathibitisha. Hivi karibuni, Mswanyama ameitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma na bila aibu akawaambia uongo kuwa Chama cha Walimu Tanzania kinamiliki hisa 99 za Kampuni ya Teachers Development Company Limited (TDCL), ...

Read More »

Bilionea Monaban wa CCM apata pigo

Mfanyabiashara bilionea Dk. Philemon Mollel, anayemiliki kampuni ya Monaban Trading and Farming Co. Limited, amepokwa kinu kilichokuwa mali ya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) jijini Arusha. Pamoja na kunyang’anywa kinu hicho, Dk. Mollel ambaye ni kada na mfadhili wa Chama Cha Mapindizi (CCM), ametakiwa alipe Sh bilioni 16 za malimbikizo ya ada ya pango kwa muda wote aliokuwa na ...

Read More »

CWT kwawaka

Fukuto limezidi kuwa kubwa ndani ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa za kuwapo ufujaji wa mali za walimu wiki iliyopita, JAMHURI linathibitisha. Wiki iliyopita JAMHURI lilichapisha orodha ya wafanyakazi waliopewa ajira kwa njia ya upendeleo ndani ya CWT, hali inayotajwa kuwa imefungua ‘kabrasha la madudu’ yanayofanyika ndani ya CWT. Haraka baada ya habari hiyo ...

Read More »

Ufisadi, upendeleo CWT

Hali si shwari katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kwani wakubwa wa chama hicho kwa sasa wanatazamwa kwa jicho la kutiliwa shaka katika uadilifu wao baada ya kutumia ukabila, udugu na upendeleo wa kila aina kuendesha chama hicho, JAMHURI limebaini.  Tuhuma kadhaa zimeelekezwa kwa viongozi wa chama hicho, hasa Katibu Mkuu, Deus Seif. Miongoni mwa tuhuma hizo ni pamoja na ...

Read More »

Masele yametimia

Hatima ya Stephen Masele kuendelea au kutoendelea kuwa mbunge katika Bunge la Afrika (PAP) inajulikana wiki hii. Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekaliwa vibaya kisiasa, na aliyeshika mpini kwenye vita hiyo ni Spika Job Ndugai ambaye naye anatoka katika chama hicho. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa ni Makamu wa ...

Read More »

Wamdanganya Magufuli

Kashfa imegubika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi mwaka huu yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya. Kashfa hiyo imekikumba Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU). Ndani ya chama hicho, baadhi ya viongozi wake wanadaiwa kuwasilisha jina la kigogo asiyestahili kuwa mfanyakazi bora, akapewa mkono na Rais Dk. John Magufuli na kukabidhiwa cheti cha mfanyakazi bora na zawadi ya ...

Read More »

Mazito ya Mengi

Mfanyabiashara maarufu nchini na kimataifa, Reginald Mengi, amekuwa na maisha yenye mengi, kuanzia mwenendo wake binafsi na mwenendo wake ndani ya jamii alimoishi. Undani wa maisha yake umejibainisha katika kitabu chake cha hivi karibuni kinachoitwa “I Can, I Must, I Will” chenye kaulimbiu ya “The spirit of success”. Mengi, katika kitabu hicho amepata kukizungumzia kifo, hasa baada ya kufariki dunia ...

Read More »

CCM: CAG safi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema ukaguzi na udhibiti wa ndani ya chama hicho kwa sasa ni zaidi ya kile kilichobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Kwa mujibu wa Dk. Bashiru, Kamati ya Kuhakiki Mali za CCM aliyoiongoza kwa takriban miezi mitatu ilibaini mengi zaidi ...

Read More »

CUF njia panda

Wabunge 24 wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye amehamia Chama cha ACT – Wazalendo, wataendelea kushikilia ubunge wao hali inayoiweka CUF njia panda, JAMHURI limeelezwa. Wabunge hao walijikuta katika mtihani wa kuchagua ama kuachana na ubunge wao wamfuate Maalim Seif ACT au wabaki CUF kulinda ubunge wao hadi ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons