Biashara

JPM ABAINI AIRTEL NI MALI YA SERIKALI KWA ASILIMIA 100

RAIS John Magufuli amesema Serikali imebaini kuwa kampuni ya Mawasiliano ya Bharti Airtel ni mali ya Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL) kumwagiza Waziri wa fedha na mipango kufuatilia suala hilo haraka ili Airtel irudishwe kumilikiwa na serikali. Rais ameyasema hayo leo Desemba 20 wakati akizungumza kwenye Ofisi za Taifa za Takwimu mjini Dodoma. “Kampuni ya AIRTEL imethibitika kuwa ni mali ...

Read More »

Airtel Yaleta Bando Mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ MPYA

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari. Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Isack Nchunda akisikiliza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani). Viongozi hao wakiwa wameshikilia bango la kifurushi cha 1GB ya Yatosha Intaneti kilichozinduliwa. Dar es salaam,  Desemba 12, 2017: Airtel Tanzania mtandao bora kwa Smartphone yako ...

Read More »

Ukweli Kuhusu Soko la Muhogo China

Sasa mkulima au mfanyabiashara akitaka kuuza au kununua muhogo, ni lazima aelimishwe juu ya masharti hayo ya mkataba. Mwenye dhamana ya kutoa elimu hiyo ni nani? Kwa maoni yangu ni Wizara ya Kilimo ambayo ndio imeingia mkataba na Mamlaka za China, mkataba huo uliosainiwa una kipengele kimoja kinachosema mtu au kampuni yoyote yenye nia ya kuuza muhogo kwenye soko la ...

Read More »

NUNUA LUKU KWA NJIA ULIYOZOEA BAADA YA MAREKEBISHO SASA MAMBO POA

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) Tunawataarifu Wateja wetu kuwa, hivi sasa mifumo ya LUKU inapatikana katika njia zote za manunuzi. Wateja mnaweza kufanya manunuzi kwa kutumia njia zote. Asanteni kwa ushirikiano wenu. Tovuti: www.tanesco.co.tz Mitandao ya Kijamii www.facebook/tanescoyetultd twitter.com/tanescoyetu Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu Desemba 10, 2017

Read More »

Magufuli: Naombeni Kampuni ya Total Mharakishe Ujenzi Bomba la Mafuta

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na viongozi wa kampuni ya Total ambayo ni mwekezaji mkubwa wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania na kuwahakikishia kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kwa kampuni hiyo na washirika wengine katika ujenzi wa ...

Read More »

Chama Cha Maofisa Uhusiano Chazinduliwa Dar

CHAMA Cha Maofisa Uhusiano wa Umma (PRST) kimezinduliwa jijini Dar es Salaam, ambapo maudhui makubwa ya kuundwa kwa umoja huo ni kutambulika rasmi kama taasisi na kupanuana mawazo ya utumishi miongoni mwa wanachama, ikiwa ni pamaoja na kuendesha shughuli zao kwa utaratibu maalum. Akihutubia katika uzinduzi huo, mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ...

Read More »

AGPAHI yamwaga misaada Shinyanga

Shirika la AGPAHI, linalojihusisha na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI, limezindua majengo mawili kwa ajili ya Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na vimelea hivyo.   Shirika hilo linalofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimarekani (CDC) nchini Tanzania, limezindua majengo hayo kwenye Zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama, na Kituo cha Afya ...

Read More »

GST yaongeza thamani madini ya nikeli

Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kupitia maabara yake ya utafiti wa madini, imefanikiwa kuongeza thamani ya madini ya nikeli (Ni) kutoka katika mbale za Milima ya Mahanza-Haneti mkoani Dodoma.   Akizungumza na MEM Bulletin, Mhandisi Priscus Kaspana, mmoja wa wanajopo la watafiti kutoka GST, anasema kuwa utafiti huo ulianza Machi 2015, na tayari sampuli nne zimefanyiwa utafiti wa uongezaji thamani ...

Read More »

Nguvu ya mawazo katika mafanikio kiuchumi

Kila kitu kinachoonekana duniani kilianza na mawazo. Mawazo ndiyo kiwanda kikubwa cha uumbaji wote unaoonekana duniani. Hata katika vitabu vya dini tunaelezwa kuwa Mungu aliamua (Mawazo) kuumba mbingu na nchi. Ninaposoma Biblia kuhusu habari hizi za uumbaji wa Mungu, kuna kitu huwa najifunza kwa namna ambavyo Mungu aliumba mbingu na nchi. Kimsingi Mungu aliamua kuumba dunia hii pamoja na vyote ...

Read More »

Wafanyakazi ndiyo injini katika ujasiriamali

Mwishoni mwa Februari mwaka huu nilikuwa nikisafiri kutoka Wilaya ya Mvomero kuelekea Kilombero mkoani Morogoro. Nilipofika Morogoro mjini niliingia kwenye basi moja ambalo linafanya safari zake kati ya Morogoro mjini na Ifakara.  Muda niliokata tiketi katika basi hilo ilikuwa ni saa tisa na nusu jioni, lakini ndani ya hilo basi nilikutana na abiria ambao walikata tiketi majira ya saa tatu ...

Read More »

Ripoti yabaini madudu zaidi TRL

Ripoti ya awali kuhusu uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa mabovu uliofanywa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), imebaini kuwa menejimenti ya kampuni hiyo haikuwa makini kushughulikia maombi ya kuongezewa muda, yaliyowasilishwa na Kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Limited ya nchini India.   Uchunguzi umebaini kuwa mkataba wa zabuni namba PA/113/2012-13/ME/G/OE/014 ya ununuzi wa mabehewa 274 ya mizigo, Kampuni ...

Read More »

‘Serikali imekurupuka, imeumbuka’

Serikali imeingia doa. Migomo wafanyabiashara na madereva wanaoendesha mabasi ya abiria, imetikisa nchi kiasi cha kufanya wadau kadhaa kueleza kuwa nchi imekosa sifa za uongozi. Tukio la kwanza, ambalo limekuwa likijirudia linahusu wafanyabiashara ambao mara kwa mara wamekuwa wakigoma kwa kufunga maduka kwa shinikizo la kuachiwa Mwenyekiti wao, Johnson Minja. Tukio la pili ni la madereva, ambao Ijumaa iliyopita walitekeleza ...

Read More »

Wateja wa ulimwengu mpya wa biashara

Katika makala mbili zilizopita nilikuwa nikichambua kuhusaina na ulimwengu mpya wa biashara. Nilieleza kwa kina namna uchumi ulivyohama kutoka viwanda kwenda taarifa na huduma, na hivyo kuathiri namna biashara zinavyofanyika. Katika makala zile mbili nilieleza kwa sehemu kubwa kuhusu taarifa zinavyoathiri mienendo ya biashara. Katika makala hii leo ninamalizia kwa kuangalia uchumi wa huduma lakini mahususi tunaangalia kizazi cha wateja ...

Read More »

Nauli za daladala kushuka Machi 18

Nauli za daladala nchini zinatarajia kushuka mwishoni mwa mwezi huu kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta nchini na duniani kwa ujumla.   Mwenyekiti  wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DRCOBOA), Sabri Mabrouk, ameiambia JAMHURI kuwa wamiliki wa daladala watakumbwa na “msiba mkubwa hivi karibuni” kutokana na msimamo wa Serikali ambayo inatarajia kushusha nauli kutokana ...

Read More »

PPF yafafanua michango ya zamani

Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) umewatoa wasiwasi wafanyakazi wa mashirika ya umma waliochangia tangu mwaka 1978, kwa michango isiyoonekana kwenye mtandao wa mfuko huo.

Read More »

Rushwa yazigonganisha Mahakama, Wizara

Wizara ya Nishati na Madini imeingia kwenye mvutano na Mahakama baada ya mhimili huo kuamuru raia wa China aliyekamatwa akitorosha madini ya tanzanite, arejeshewe madini hayo kinyume cha sheria.

Read More »

DECI mpya yaibuka Dar

Kituo cha Mafunzo ya Ujasiriamali Tanzania kilichopo jijini Dar es Salaam, kimeingia katika kashfa ya kuwatapeli wajasiriamali walioshiriki katika semina  za ufugaji kwa kuwapa ahadi hewa.

Read More »

CIDTF: Korosho inaweza kuwainua wakulima

Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini. Kwa sasa zao hili hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga.

Read More »

Edwin Butcher: Hatuhusiani na Dk. Amani

Mmiliki wa duka la nyama linaloitwa Edwin Butcher la Rwamishenye, Bukoba, amejitokeza na kusema kuwa bucha yake haina uhusiano wowote na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Bukoba, Dk. Anatory Amani, au udini kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.

Read More »

Mapapa wa ‘unga’ watajwa

*Kinondoni, Magomeni, Mbezi, Tanga watia fora

*Wamo Wakenya, Wanigeria, waimba taarab Dar

*Wengine wapata dhamana kimizengwe, watoroka

Vita dhidi ya wauzaji na wasafirishaji dawa za kulevya inazidi kupamba moto, na sasa JAMHURI imepata orodha ya watu wengine 245 wanaotajwa kuwa ndiyo ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu hapa nchini.

Read More »

Wauza unga 250 nchini watajwa

*Soma orodha uone maajabu, wamo masheikh, wachungaji

*Wengi wanatoka Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, Morogoro

*Mahakama yawaweka chini ya uangalizi, wanaripoti polisi

Majina ya Watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamejulikana, na JAMHURI imeamua kuyachapisha. Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wamo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada, huku wengine wakijifanya ni wazee wa kanisa na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

Read More »

Ulaji wa mpya waibuliwa

*Malipo ya ndege utata mtupu

*Wahusika wakalia kuti kavu

*Waziri Membe aingilia kati

 

Kukiwa na taarifa kwamba uongozi wa juu serikalini umeagiza kuchunguza ulaji wa mamilioni ya shilingi wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue), siri nzito za ufisadi zimeendelea kuanikwa.

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons