Habari za Kitaifa

Ngorongoro inavyotafunwa

Wakati Rais Dk. John Magufuli akihimiza kubana matumizi ya idara na taasisi za serikali, hali ni tofauti kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Shilingi bilioni 1.1 zimetumika kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 kuhudumia vikao vya bodi hiyo. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, bodi imekaa vikao 20 tofauti na utaratibu unaoagiza vikao viwe vinne kwa ...

Read More »

Aibu Mkwakwani

Mpita Njia (MN) anatanguliza salamu zake za Sikukuu ya Pasaka kwa Wakristo wote nchini ambao bila shaka wataungana na wenzao wa maeneo mengine duniani kwa ajili ya siku hiyo ya kiimani kwao. Tukiachana na hayo, kama ilivyo kawaida yake, MN wiki hii alikuwa mkoani Tanga kwa ajili ya shughuli zake za ujenzi wa taifa. Loh! Tanga kuna mengi yaliyo mazuri, ...

Read More »

Jiji waomba fursa mabasi 100 ‘mwendokasi’

Uongozi wa Jiji la Dar es Salaam umeiomba Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwapa kibali cha kuongeza mabasi ya usafiri wa haraka (mwendokasi) katika Jiji la Dar es Salaam. Lengo la kuomba kibali hicho ni kutaka kushirikiana na mkandarasi aliyepewa dhamana ya kuendesha mradi huo ili kuboresha huduma ya usafiri ya ...

Read More »

Nondo feki zazua balaa Siha

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) imeanza uchunguzi kuhusu tuhuma zinazoikabili kampuni moja ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi mkoani Kilimanjaro, inayodaiwa kuiuzia serikali nondo feki zisizo na ubora. Kampuni hiyo ambayo kwa sasa jina lake tunalihifadhi baada ya mkurugenzi wake kutopatikana, ilishinda zabuni ya kuuza nondo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha ...

Read More »

‘Tunateseka’

Mahabusu wawili wamemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, wakidai wanashtakiwa kwa kosa la kuua ilhali aliyefanya mauaji hayo na kukiri yuko huru uraiani. Michael Laizer na Lucas Mmasi, wanashikiliwa katika Gereza Kuu Mkoa wa Arusha, Kisongo, tangu mwaka 2015 wakikabiliwa na shtaka hilo wanalodai kuwa ni la kubambikiwa. Barua hiyo ambayo JAMHURI imeona nakala yake, ...

Read More »

‘Mjadala wa CAG, Bunge si utekelezaji wa ilani’

Mpita Njia, maarufu kwa ufupisho wa MN, kwa wiki nzima iliyopita amesikia mijadala mingi katika mitaa kadhaa aliyopita wakati wa shughuli zake za kawaida za kila siku. Mijadala hii ilihusu Azimio la Bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Bunge limeazimia kutokufanya kazi na msomi ...

Read More »

Rais Magufuli azima umegaji hifadhi

Rais John Magufuli amekataa mapendekezo ya wanavijiji katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, ya kutaka wamegewe ardhi katika Pori la Akiba la Selous. Amewaonya wanasiasa ambao hutumia ghiliba wakati wa kampeni kwa kuahidi kuwa wakichaguliwa watahakikisha wanamega maeneo ya hifadhi na kuwapa wananchi. Rais Magufuli yumo katika ziara ya siku tano mkoani Ruvuma. Amesema Tanzania ina ardhi kubwa ambayo ikitumiwa ...

Read More »

BoT wamtosa mteja aliyeibiwa Ecobank

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema haiwezi kufanya chochote kumsaidia mfanyabiashara aliyeibiwa fedha kwenye akaunti yake katika Ecobank, Tawi la Uhuru, jijini Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) imeitia hatiani Ecobank Tanzania Limited kwa kumwibia mteja wake, Kampuni ya Future Trading Limited, Sh milioni 66 kutoka kwenye akaunti yake. Fedha hizo zimeibwa kwenye akaunti hiyo kupitia ...

Read More »

Tuhuma za ufisadi zatanda Kwimba

Kumeibuliwa tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza. Miradi mitano ya ujenzi imekwama. Miradi iliyokwama ni ujenzi wa vyumba vya maabara wa mwaka 2014; kliniki ya mifugo na bwalo la chakula, iliyoanza mwaka 2016. Mingine ni ujenzi wa nyumba tatu za walimu katika shule za msingi za Itegamatu, Ilula na ...

Read More »

Jaji azuia waandishi kuripoti kesi ya mauaji

Jaji Firmin Matogolo anayesikiliza shauri la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ya Himo, Humphrey Makundi, ameingia kwenye mvutano na waandishi wa habari wanaoripoti kesi hiyo baada ya kuwapiga marufuku kutonukuu chochote juu ya mwenendo wa shauri hilo. Badala yake, jaji huyo kutoka Mahakama Kuu Divesheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi akawataka waandishi hao kuingia ...

Read More »

Mkakati kuing’oa CCM mwaka 2020

Mnyukano wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza. Vyama 10 vya upinzani vimeandaa mkakati wa kisayansi kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutumia Sheria mpya ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2018. Kwa upande wake, CCM imejigamba kuwa maisha ya vyama vya upinzani katika uwanja wa siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao nchini ni ‘mahututi’. Gazeti la JAMHURI linafahamu kwamba vyama ...

Read More »

Ecobank yamwibia mteja mamilioni

Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) imeitia hatiani Ecobank Tanzania Limited kwa kumwibia mteja wake, Kampuni ya Future Trading Limited, Sh milioni 66 kutoka kwenye akaunti yake. Fedha hizo zimeibwa kwenye akaunti hiyo kupitia huduma ya internet banking na kuziingiza katika akaunti iliyoko nchini Afrika Kusini. Hukumu hiyo ya kesi namba 68 ya mwaka 2014, imetolewa na Jaji Barke Sehel. Inahusu ...

Read More »

Rais ampandisha cheo aliyekataa rushwa

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo, ameteuliwa kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, imesema uteuzi huo uliofanywa na Rais John Magufuli, umeanza Machi 31, mwaka huu. Desemba, mwaka jana, Gazeti la JAMHURI liliandika habari iliyohusu Mbibo kukataa rushwa. Baadaye Januari, mwaka huu ...

Read More »

KNCU, Lyamungo AMCOS wavutana umiliki shamba la kahawa

Mvutano mkali umeibuka baina ya Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU) na Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) cha Lyamungo kuhusu umiliki wa shamba la kahawa la Lyamungo kutokana na kila upande kudai ni mmiliki halali. Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 112 lililopo Lyamungo, Wilaya ya Hai limekuwa katika mgogoro usiokwisha kwa muda wa miaka 16 hadi sasa, hivyo ...

Read More »

Serikali yashitukia ufisadi wa milioni 71/-

Serikali imeshitukia matumizi mabaya ya fedha za makusanyo ya ardhi kiasi cha Sh milioni 71. Fedha hizo zinazodaiwa kutojulikana zilipo zinatokana na malipo ya viwanja 194 vya wakazi wa mji wa Hungumalwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza. Raia hao walitoa fedha hizo ili wapimiwe na kupewa hati za maeneo yao ya makazi na biashara. Naibu Waziri wa ...

Read More »

Polisi ‘yamtimua’ askari aliyekamata mihadarati

Jeshi la Polisi limemtimua kazi askari wake, Manga Msalaba Kumbi, mwenye namba F. 5421, kwa kile kinachodaiwa ni mwenendo mbaya kazini. Askari huyo alikuwa anafanya kazi mkoani Mwanza. Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba askari huyo alikumbwa na masahibu hayo baada ya kukamata mihadarati inayohusishwa na ‘wakubwa’ ndani ya Jeshi la Polisi. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, askari huyo ...

Read More »

Aliyepigwa risasi Ikulu Ndogo kuburuzwa kortini

Mtu mmoja aliyepigwa risasi na polisi akiwa maeneo ya Ikulu Ndogo inayotumiwa na Makamu wa Rais jijini Mwanza atafikishwa mahakamani baada ya matibabu. Raia huyo amelazwa Hospitali ya Rufaa mkoani hapa ya Sekou Toure akiendelea kuuguza jeraha la risasi mwilini mwake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, amelithibitishia Gazeti la JAMHURI akisema tukio hilo limetokea Machi 11, 2019 ...

Read More »

Wagombea msikiti aliojenga Nyerere

Waumini wa Kiislamu katika Kijiji cha Butiama na uongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mara wamo kwenye mgogoro kuhusu umiliki na uendeshaji wa msikiti uliojengwa kwa msaada wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kijijini hapo. Msikiti huo ulianza kujengwa wakati Mwalimu akingali hai, na ulifunguliwa rasmi na aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Omar Ali Juma, ...

Read More »

Gari la Polisi ladaiwa kuua bodaboda Segerea

Gari la Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadaiwa kuua dereva wa pikipiki, Cosmas Swai (42), kwa kumkanyaga kichwani akiwa amembeba mkewe, Anna Swai (39) pamoja na mwanawe, David Swai (11). Ajali hiyo imetokea Machi 12, mwaka huu, eneo la Segerea Mbuyuni, baada ya mashuhuda wa ajali hiyo kudai kuwa gari hilo ...

Read More »

Magufuli kutua China

Rais Dk. John Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuvuka mipaka ya Bara la Afrika, kwa kuitembelea China kwa ziara ya kiserikali, Gazeti la JAMHURI limebaini. China imekuwa mdau muhimu wa maendeleo wa Tanzania, kupitia mkakati mahususi wa Tanzania ya viwanda, wawekezaji kadhaa kutoka nchi hiyo ya barani Asia wameitikia wito kwa kuanzisha viwanda kadhaa hapa nchini. Vyanzo vyetu vinasema ...

Read More »

Katavi, Tabora vipi?

Mpita Njia ameshitushwa na taarifa za hivi karibuni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshika nafasi ya tatu barani Afrika katika ndoa na mimba za utotoni. Hizi si tu ni taarifa za kushitua, bali ni taarifa za aibu katika wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano inajielekeza katika kuhimiza elimu kwa wote, kiasi cha kuondoa malipo ya ada. Hili ...

Read More »

Ajali ya ndege yaua abiria wote

Watu wote 157 waliokuwa safarini katika ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia,  Boeing 737, wamepoteza maisha baada ya ndege hiyo kuanguka. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kuelekea mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumapili iliyopita. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ethiopia, abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo ni 149 na watu wengine wanane ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons